Thursday, January 17, 2013

WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA KULA UYOGA


Abdul Bandola na Edilitruda Chami

Watu watatu wa familia moja wamefariki dunia katika kijiji cha Itigi wilaya ya Manyoni Mkoani Singida baada ya kula uyoga unaosadiki kuwa na sumu.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoa wa Singida ACP Linusi Sinzumwa  amesema tukio hilo limetokea  tarehe 15 Januari 2013.

Amesema mwanamke mmoja ambaye ametambuliwa kwa jina la Agnes Muna mwenye umri wa miaka 19 alipika uyoga  aliouchuma shambani mwake kwa ajili ya kitoweo na kwa cha famillia pasipo kujua kama una sumu.

Kamanda Sinzumwa amesema baada ya muda mfupi watoto walianza kutapika na kuishiwa nguvu ndipo walipopelekwa katika hospitali ya wilaya ya Manyoni kupatiwa matibabu lakini walifariki dunia.

Amewataja waliokufa kuwa ni  Yese Jeremia mwenye umri wa miaka 6, Joshua Jeremia mwenye umri wa miaka 3 pamoja na mama yao  Agnes Muna aliyefariki baadaye

Jeshi la polisi mkoani Singida kwa kushirikiana na mkemia mkuu wa serikali wanaendelea na uchunguzi kujua aina ya sumu inayotajwa kuwemo katika uyoga huo.

No comments: