Tuesday, January 15, 2013

UBUNIFU WA KIUCHUMI MKOANI SINGIDA

Na, Debora Marco
SR fm




Mkazi wa manspaa ya Singida Bwana Thomas Taghama akijishughulisha na ujasiriamali kwa kuengeneza na kuuza viatu vya asili maarufu kwa jina la masendeu katika eneo la maabara mkoani Singida.

Katika mkoa wa Singida viatu vya asili  vimekuwa  kivutio  kikubwa  nchini kwa ujumla hasa kwa wageni wanao toka nchi mbalimbali wanaotembelea mikoa ya kanda ya kati.

Vile vile swala la ajira zisizo rasmi limekuwa likishika kasi kutokana  na uhaba wa ajira hivyo kupelekea wananchi kuamua kujiariri wao wenyewe ili kujipatia kipato.

 

No comments: