Wednesday, January 16, 2013

WACHUUZI WA VITUNGUU SINGIDA WAHAMISWA


Na Beatrice Mosses.

 
Manispaa ya Singida imewaamuru wafanya biashara wa soko la vitunguu la Ukombozi Singida Mjini kuhamia katika eneo la Misuna.

Mkurungenzi wa manispaa ya Singida Bw. Mathias Mwangu ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wafanya biashara hao, kuwa eneo hilo limekuwa dogo na bidhaa ni nyingi.

 Amesema zao la vitunguu linahitaji eneo kubwa kwa ajili ya kuanika, lakini kutokana na wingi wa zao hilo eneo hilo limeonekana kutokidhi mahitaji.

Baadhi ya wafanya biashara wa zao hilo wameiomba Manispaa iwajengee vibanda hata viwili vitakavyotumika kulipia ushuru.

Hata hivyo miundombinu katika soko la Misuna kama vyoo na vibanda bado havijakamilika, Bw. Mwangu amesema Manispaa itakamilisha miundombinu hiyo haraka ili soko la Misuna lianze kutumika.

Soko la Ukombozi litaendelea kuwepo kwa ajili ya kuuzia kuku na bidhaa nyingine ndogondogo.  

No comments: