Tuesday, January 29, 2013

DODOMA KUZIMA MITAMBO YA ANALOGIA


Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imekamilisha maandalizi ya kuzima mtambo wa mawasiliano wa analogia na kuwasha mtambo mpya wa digital mkoani  Dodoma.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa utangazaji TCRA Bw. Habi Gunze wakati akizungumza na waandishi wa habari jana ambapo amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya maandalizi ya kuwasha mtambo huo unaotarajiwa kuwashwa usiku wa alhamisi ya wiki hii kukamilika.

Amesema mwezi mmoja sasa umepita tangu jiji la Dar es salaam limehama kutoka mfumo wa analogia na kwenda digitali hivyo kwa sasa ni zamu ya mkoa wa Dodoma na Tanga.

Naye Meneja wa TCRA Bw. Innocent Mungi amewataka wakazi wa mkoani humo kuhakikisha kuwa wamenunua ving’amuzi ili kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza.

Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Dodoma wameipongeza mamlaka husika kwa kufikia hatua hiyo wakati wengine wakilalamikia gharama za matangazo kwani watatakiwa kulipia.   EndS

1 comment:

Unknown said...

Habari za majukumu,
Pia poleni na kazi,na hongereni kwa usikivu mzuri wa Matangazo yenu