Friday, January 25, 2013

MANSPAA YA SINGIDA YALAUMIWA KUTWAA ARDHI YA WANANCHI


Wakazi wa vitongoji vya Mwamtanda na Mwaja kata ya Mandewa wameilalamikia halmashauri ya Manispaa  ya Singida  kwa kutotimiza ahadi ya kuwalipa fidia waliyoitoa wakati  maeneo yao  ya  ardhi  yalipochukuliwa na serikali  kwa ajili ya upimaji wa viwanja vipya.

Wakazi hao wamesema hayo jana wakati  wakizungumza na Mkuu wa wilaya ya Singida  Bi. Queen Mlozi, baada ya kutembelea vitongoji hivyo.

Wakazi hao wamesema,  wakati serikali inahitaji viwanja  waliahidiwa kuwa kila mtu  atapewa kiwanja na kulipwa fidia jambo ambalo halikutekelezwa, hali  iliyopelekea baadhi ya wananchi kukosa makazi.

Wamesema  baadhi yao wamekwenda  katika ofisi za ardhi ili  kutaka kupata maelekezo zaidi na kuonyeshwa sehemu  mbadala na kufuatilia fidia  zao, badala yake  wamepewa  barua za kutakiwa kuondoka katika maeneo yao.

Mkuu wa  wilaya  ya Singida  Bi.  Mlozi  amewataka wakazi hao kuwa na subira kwa kuwa suala hilo linatafutiwa ufumbuzi.

No comments: