Friday, January 18, 2013

STANDARD RADIO YAANZA VIPINDI NA HABARI




 

 
 
 
Pichani: Ndg. Prosper kwigize, Mratibu mradi wa Standard Radio fm, iliyopo Mjini Singida nchini Tanzania.
Mratibu wa maradi wa Standard Radio iliyopo mjini Singida Bw. Prosper Kwigize ametoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Singida na mikoa jirani inakosikika redio hii, kuitumia ipasavyo kwa kushiriki kikamilifu katika kuandaa vipindi mbali mbali na  kutoa maoni yao na kupitia chombo hiki cha habari.
Bw. Kwigize ametoa wito huo jana, wakati akiutangazia umma kuwa sasa Standard redio imeanza rasmi kutangaza habari pamoja na vipindi  ambavyo vitalenga sekta mbali mbali katika jamii. 
Amesema endapo wakazi wa mkoa wa Singida watakitumia ipasavyo chombo hiki cha habari watajiletea maendeleo pamoja na kutafuta ufumbuzi wa martatizo yanayowakabili kwani mawasiliano ni nyanja muhimu katika jamii.

1 comment:

Prosper Ngairo said...

Hongera sana wajina,juhudi zako tunaziona na tunazidhamini sana.