Wednesday, January 9, 2013

MITI MILIONI 2 YAPANDWA SINGIDA


HALIMA JAMAL


HALMASHAURI ya manispaa ya Singida,imepanda miti 2,645,314 ya aina mbalimbali katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa manispaa ya Singida, Bw. Mathias Mwangu,wakati akitoa taarifa ya mazingira siku ya uzinduzi wa upandaji miti katika manispaa hiyo.

Bw. Mwangu amesema zoezi la upandaji miti lengo lake ni kuzuia mmomonyoko wa ardhi na kudhibiti kuenea kwa jangwa pamoja na kufanikisha upatikanaji wa kivuli, matunda, kuni na mbao.

Ametaja faida nyingine za miti kuwa ni kuhifadhi na kutunza vyanzo vya maji na kupendezesha mji na kuweka madhari nzuri.

Amesisitiza kuwa ili kufanikisha ni kuhamasisha upandaji miti kwa kuongeza uzalishaji wa miche ya miti katika kila irada.

wakuu wa idara 13 wa manispaa,wameotesha miche ya miti 13,000 ya aina mbalimbali ambayo imeoteshwa kwenye kitalu kilichopo kwenye eneo la ofisi kuu.

Aidha,mkurugenzi huyo alisema manispaa imetenga jumla ya shilingi 3,200,000 kwa ajili ya kuotesha miche zaidi ya 15,000 katika kata za Mwankoko,Uhamaka, Mtipa na Mandewa.

No comments: