Tuesday, January 1, 2013

BEST WISHES FROM MANAGING DIRECTOR

 


On my behalf, Management and staff of STANDARD VOICE LTD & STANDARD RADIO FM 90.1 Singida, I hereby wish all listeners, Singida community and all Tanzanians a HAPPY & PROSPEROUS NEW YEAR 2013.

MPENDWA MSIKILIZAJI WA STANDARD RADIO FM

MIMI JAMES JAPHET DAUD, MKURUGENZI MTENDAJI WA MAKAMPUNI YA BUHANZO INTERPRISES LTD NA STANDARD VOICE LTD AMBAYE NI MMILIKI WA STANDARD RADIO FM SINGIDA

NINAPENDA KUCHUKUA FURSA HII KUKUPONGEZA SANA KWA KUUFIKIA MWAKA MPYA WA 2013, NINAWAOMBEA MWAKA HUU UWE WA AMANI, FURAHA, UPENDO NA UCHAPA KAZI UTAKAOLETA TIJA KWA MAENDELEOO YA MTU MMOJA MMOJA, KAYA, MKOA NA TAIFA KWA UJUMLA

MIMI PAMOJA NA WAFANYAKAZI WOTE WA MAKAMPUNI YA BUHANZO NA STANDARD, TUNAPENDA KWA NAMNA YA PEKEE KABISA KUTOA SHUKURANI ZA DHATI KWAKO WEWE MSIKILIZAJI WA STANDARD RADIO, WAKAZI WOTE WA MKOA WA SINGIDA, UONGOZI WA SERIKALI, MASHIRIKA YA UMMA NA TAASISI ZA KIJAMII PAMOJA NA VYAMA VYOTE VYA SIASA, KWA NAMNA MNAVYOIPOKEA NA KUISIKILIZA RADIO YETU.

NDUGU ZANGU UKARIMU WENU KWA STANDARD RADIO NI WA KIPEKEE KABISA, NINAPENDA KUKIRI KUWA UAMUZI WETU WA KUILETA RADIO HII MKOANI SINGIDA UMEENZIWA NA WANA SINGIDA VILIVYO, TUMEKUWA TUKIPOKEA MAONI MENGI AMBAYO YOTE YANADHIHIRISHA MAPENZI MEMA KWA RADIO HII

STANDARD RADIO NI RADIO YA JAMII, YENYE MALENGO YA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JAMII KWA NJIA YA KUHABARISHA, KUELIMISHA NA KUBURUDISHA, MALENGO YETU NI KUISAIDIA JAMII KUIBUA NA KUTEKELEZA SHUGHULI ZA MAENELEO HUSUSANI KILIMO, BIASHARA, UJASIRIAMALI PAMOJA NA KUHIMIZA MASUALA YA ULINZI NA USALAMA KUPITIA KAULI MBIU YA ULINZI SHIRIKISHI NA UTII WA SHERIA BILA SHURUTI

JAMII INAPASWA KUPATA FURSA YA KUTOA YALIYO MOYONI ILI VYMBO VYA MAAMUZI VIYASIKIE NA KUYAFANYIA KAZI, JAMBO HILI NI GUMU KAMA HAKUNA CHOMBO MBADALA CHA KUFIKISHA SAUTI YA WANANCHI. HII NDIYO SABABU SISI TUMEKUJA SINGIDA ILI TUWE SAUTI YA WASIO SIKIKA, KAMA KAULI MBIU YETU INAVYO SEMA (THE VOICE OF VOICELESS)

STANDARD RADIO BADO IKO KATIKA MCHAKATO WA MWISHO KUELEKEA KUANZA MATANGAZO RASMI KWA MUJIBU WA TARATIBU ZA MAMMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA, KWA HIYO TUNAKUOMBA NDUGU MSIKILIZAJI UENDELEE KUWA NA SUBIRA KWANI WAKATII WOWOTE MATANGAZO YETU YATAANZA KUSIKIKA KWA NJIA YA VIPINDI MBALIMBALI.

SUBIRA YAVUTA KHERI, TUMEVUMILIA TANGU ENZI ZA UKOLONI NA BAADA YA UHURU MIAKA HAMSINI ILIYOPITA SINGIDA IKIWA HAINA RADIO, SASA TUSISHINDWE KUVUMILIA KIPINDI HIKI KIFUPI KIJACHO AMBACHO  STANDARD RADIO INAJIWEKA SAWA ILI KUKULETEA MATANGAZO KAMILI

NARUDIA TENA KUKUSHUKURU NA KUKUTAKIA MWAKA MPYA MWEMA

 
MUNGU AWABARIKI

No comments: