Wednesday, January 16, 2013

TASWA WAUNDA TIMU


Chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania {TASWA} kisiwani Zanzibar kimeunda timu ya soka itakayojumuisha waandishi wa habari za michezo na burudani

 

Akizungumza na waandishi wa habari katibu wa chama hicho Donisya Thomas amasema kuwa wachezaji wa timu hiyo watakuwa wale waliojiunga na chama hicho tuu,na kwamba madhumuni ya kuunda timu hiyo ni kudhihirisha kwa vitendo kuwa waandishi wa habari na wao ni wanamichezo hodari  na siyo waandishi wa habari za michezo pekee

 

Aidha amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kuwapa furksa zaidi wanamichezo ya kuweza kuwa na afya njema ya wanachama wao na kwamba  wanataswa watatambulika kitaifa na kimataifa

 

Pamoja na hayo katibu huyo amesema kuna changamoto zinazowakabili kama vile ukosefu wa vifaa vya kufanyia mazoezi,jezi na mahitaji mengine yanayohitajika wakati wa michezo

 

Timu hiyo kwa sasa itakuwa chini ya kocha wake Ali Bakari Cheupe,ambapo katibu ni Ameir Khalid, mwekahazina ni mwajuma juma,mwenyekiti ni mwinyimvua Abdi Mzukwi

No comments: