Monday, January 14, 2013

TIA SINGIDA KWAWAKA MOTO-POLISI WATANDA


Chuo cha Uhasibu TIA Singida eo kimeingia katika mgogoroo wa utawala na wanachuo kufuatia uwepo kwa dosari katika uchaguzi wa viongozi wa wananchuo halii iliyopelekea jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia na vyombo vingine vya usalama kukizingira chuo hicho

Imeelezwa kuwa wanachuo hao wameamua kufanya vurugu dhidi ya uongozi baadaya aliyetangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya rais wa serikali ya wanachuo kutokuwa na sifa za ushindi kwa mujbu wa kanuni za uchaguzi wa serikali za wachachuo Tanzania

Standard Radio imeshuhudia kundi kubwa la askari polisi wenye silaha za moto na mabomu ya machozi wakiwa wametanda eneo zima la chuo hicho hicho,

Aidha wanachuo wanaonekana kukaa katika makundi makundi wakijadili na kulalamikia ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi huo.

No comments: