Wednesday, January 23, 2013

POLISI KUYAFUNGA MAKAMPUNI YA ULINZI TABORA

Na. Moses mabula

KAMANDA wa Polisi mkoani Tabora ACP Anthony Rutta amesema kuwa atayafungia kufanyakazi makampuni yote ya ulinzi mkoani humo ambayo yanashindwa kutekeleza masharti yaliyopewa na jeshi hilo.

 

Mkuu huyo wa Polisi mkoa wa Tabora amesema kwamba jeshi la Polisi lilitoa masharti kwa wamiliki wa makampuni yaho kuwa hayaruhusiwi kuajiri walinzi wasio waadilifu ambao wamekuwa wakila njama za kufanya uharifu wa wizi kwenye taasisi mbalimbali ambayo wameingia nazo mkataba wa ulinzi.

 

Akizungumza na mwandishi wa habari ofisini kamanda Ruta alikiri kuwepo kwa baadhi ya makampuni ya ulinzi ambayo hayafuati taratibu za ajira za walinzi huku akiapa kuyashughulikia ipasavyo kwakuwa baadhi ya makampuni hayo yamekuwa yakiajiri walinzi wasio na sifa na kukosa uaminifu.

 

Kuhusu matukio ya hivi karibuni ya wizi uliofanyika katika Shirika lisilo la kiserikali la Total Land care ambalo lilipata hasara ya zaidi ya shilingi mil.kumi na tatu baada ya walinzi wa kampuni ya ulinzi ya Alliance Day & Night la hapa mjini Tabora ambao wanadaiwa kula njama na kufanya wizi wa kuvunja ofisi za Shirika hilo.

 

Kamanda Rutta amesema bado Polisi wanaendelea na uchunguzi lakini mlinzi mmoja wa kampuni hiyo anayefahamika kwa jina la Said Kayungilo alitoweka kabla ya kukamatwa.

No comments: