Tuesday, January 29, 2013

MWIGULU NCHEMBA KUWASILISHA HOJA BINAFSI BUNGENI


Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi na naibu katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi Bw. Mwigulu Nchemba anatarajia kuwasiilisha hoja binafsi katika kikao cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma

Akizungumza na Standard Radio Bw. Nchemba ameitaja hoja hiyo kuwa ni kuitaka serikali kuanzisha mfuko maalumu wa elimu ya juu

Amebainisha kuwa Tanzania haina mfuko maalumu wa kuwasaidia vijana wanaojiunga na vyuo vikuu na kwamba fedha zinazotolewa na bodi ya mikopo kwa sasa haina chanzo maalumu na cha uhakika

Kuhusu tabia ya wabunge kugeuza Bunge kama sehemu ya kurushiana maneno na kusababisha vurugu, Bw. Nchemba amesema chama cha mapinduzi kimewaelimisha wabunge wake kupeleka hoja za msingi kwa ustaarabu na kuepuka vurugu
Amesisitiza kuwa Bunge ni mahali pa kwenda kujenga hoja za maendeleo ya wananchi na kwamba chanzo cha vurugu zilizokuwa zikijitokeza mwaka jana Bungeni ni wabunge kuwa na hisia za ubinafsi badala ya kufikiria taifa.

No comments: