Saturday, January 26, 2013

MOHAMED DEWJI AMWAGA MSAADA WA VITENGE SINGIDA


Na. Nathanael Limu

Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Gullam Dewji, ametoa msaada wa pea za vitenge 7,500 zenye thamani ya zaidi ya shilimi 60 milioni, kwa ajili ya kufanikisha maandalizi ya sherehe za CCM kutimiza miaka 36 toka kianzishwe.
Dewji ametoa msaada huo mkubwa na wa aina yake, baada ya kuombwa kufanya hivyo na katibu wa CCm manispaa ya Singida.
Akizungumza na WAANDISHI jana msaidizi wa mbunge Dewji, Duda Mughenyi, alisema jumla ya vikundi vya uhamasihaji 112, vimenufaika na msaada huo wa vitenge.
Alisema pamoja na vikundi hivyo, pia wajumbe wa halmashauri mkuu ya matawi, wafanyabiashara wa kuku za kienyeji soko kuu, boda boda na taasisi mbali mbali, zitanufaika na msaada huo.

“Lengo la kumwomba mbunge Dewji msaada huo wa vitenge, ni kutaka kufanikisha sherehe hizo za chama kikongwe cha CCM kutimiza miaka 36.Chama kuendelea kuwa na mshikamano kwa kipindi chote cha miaka 36, ni jambo la kujivunia na kupigiwa mfano”,alisema Duda.

Msaidizi huyo wa mbunge,alisema kwa hali hiyo, sherehe hii muhimu, ni lazima nayo ipewe heshima ya aina yake ikiwemo wanaccm na wapenzi wake, waonekane tofauti siku hiyo ya sherehe.

Katika hatua nyingine, katibu tawi la Ughaugha (CCM), Hamisi Ramadhani, alisema msaada huo wa vitenge, ni mwendelezo wa misaada mingi ya kimaendeleo anayotoa mbunge Dewji, jimboni kwake.

No comments: