Friday, January 18, 2013

MKUU WA MKOA SINGIDA ATOA AGIZO KWA WAKUU WA WILAYA


Wakuu wa wilaya zote mkoani Singida wameagizwa kuwajulisha wananchi juu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi tangu mwaka 2005 hadi mwaka 2012, kupitia vyombo vya habari vinavyowafikia wananchi kwa urahisi.

Agizo hilo limetolewa hivi karibuni na Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Ole Kone, wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa waandishi wa habari ofisini kwake.
 
Dk. Kone amesema wakuu wa wilaya wakifanya hivyo na wananchi kupewa fursa ya kutoa maoni yao, itakuwa ni njia rahisi kufikisha taarifa kwa wananchi ambao nao watatoa maoni yao moja kwa moja na kuhoji wataalam wa sekta mbali mbali juu ya utekelezaji wa ilani hiyo.

Wakuu wa wilaya zote mkoani Singida wameahidi kutoa taarifa za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika wilaya zao kutumia vyaombo vya habari.

No comments: