Thursday, September 26, 2013

ALAT MKOANI SINGIDA WATAKIWA KUKUSANYA MAPATO YA ADA ZA LESENI

 Na.Boniface Mpagape
 Wajumbe wa  jumuiya ya tawala za mikoa Tanzania  ALAT  mkoa wa Singida wametakiwa kuonyesha  uwezo wa kukusanya  mapato yanayotokana na Ada za lesen kwa ukamirifu  ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa

Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone wakati wa ufunguzi wa Kikao cha ALAT mkoa kilichofanyika kwenye ukumbi wa parokia ya kanisa katoliki mjini Singida

Dr. Kone amesema ada za lesen zikikusanywa  kwa ukamilifu serikal itaongezea halmashauri za mkoa wa Singida wigo mpana wa vyanzo katika halmashauri zote
Amesema kwa kutumia fursa hiyo ya makusanyo kutasaidia kuwa na matokeo chanya kwa kuibua,kukusanya kusimamia na kufuatilia mapato ya halmashauri


ONGEZEKO LA WATU KATIKA MJI WA SINGIDA WAONGEZA UZALISHAJI WA TAKA LAINI NA NGUMU

Na.Edson raymond


Kuongezeka kwa idadi ya watu katika kata ya Mandewa Manispaa ya Singida kumesababisha kuongezeka kwa uzalishaji wa taka laini na ngumu katika kata hiyo na maeneo jirani.

Mwenyekiti wa kamati ya usafi na mazingira kata ya Mandewa Bw. Elifuraha Mgoma amesema hayo muda mfupi baada ya kumaliza shughuli za kufanya usafi eneo la Ginery manispaa ya Singida.

Amesema hivi sasa kunaongezeko watu lilochangiwa na taasisi za elimu kama vile vyuo, pamoja na shule jambo ambalo limepelekea kuongezeka kwa wingi wa uzalishaji wa taka katika maeneo ambayo watu hao wanaishi.

Amesema jitihada za haraka zinahitajika ili kukabiliana na tatizo hilo ikiwa ni pamoja na kujenga guba la kukusanyia uchafu kwa lengo la kuepukana magonjwa ya miripuko yanayoweza kutokea kwa sababu ya kuzagaa kwa taka



Wednesday, September 25, 2013

WAKULIMA ELFU 10 NA MIA5 KUNUFAIKA NA MRADI WA UWEZESHAJI WA FAMILIA NCHINI




Na.Mwanishi wetu

Jumla ya wakulima elfu 10 na mia 5 kutoka mikoa 15 hapa nchini wanatarajiwa kunufaika na mradi wa uwezeshaji wa familia kupitia maendeleo ya kilimo uliofadhiliwa na Bangladesh kupitia taasisi ya BRAC

Akiongea na waandishi wa habari mratibu wa mradi huo kanda ya Ziwa Bw George Zabron amesema mradi huo umeanza mwezi wa April mwaka huu ambapo kila mkulima atapatiwa mtaji kwa mwaka wa kwanza wa EURO 84
Amesema mradi huo umelenga kuleta uzalishaji kwa mkulima ambapo watajikita na ufugaji wa kuku wa kienyeji na mkulima anayelima mahindi kuanzia nusu ekari
Bw Zabron ameongeza kuwa kila mkulima atakuwa anapewa pembejeo kwa lengo la kuthibiti matumizi yasiyokuwa sahihi ya mradi huo

WANAFUNZI WAASWA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI MJINI SINGIDA



Na.  Anna Chiganga

Wanafunzi shule za sekondari mkoani Singida wametakiwa kupenda masomo ya sayansi ili kwenda sambamba na mabadiriko ya Sayansi na teknolojia
Mwalimu wa sayansi katika shule ya secondary Mitunduruni Bi.Costantini Bejimula  amesema wanafunzi wanaogopa kusoma masomo hayo kutokana na shule nyingi kutokuwa na maabara na vifaa  vya maabara  hali inayosababisha  wanafunzi kuona masomo hayo kuwa magumu
Aidha amesema wazazi wanachangia watoto wao kutopenda masomo hayo kwa kueleza kuwa ni magumu jambo ambalo si la kweli

Hatahivyo ameiomba serikali kujenga maabara na kuwakea vifaa vya maabara hatua itakayosaidia wanafunzi kupenda masomo ya sayansi

MSALABA MWEKUNDU MULEBA LATOA MABLANKET 30 KWA RAIA WA KIGENI



Na mwandishi wetu
Shirika la Msalaba Mwekundu wilayani Muleba Mkoani Kagera limetoa msaada wa mablanketi 30 kwa raia wa kigeni waliokuwa wakiishi nchini kinyume cha sheria waliotokea wilayani humo na kurejeshwa katika mataifa yao
Mkuu wa kitengo cha maafa wa shirika la Msalaba Mwekundu wilayani Muleba Bw Rafael Mbekenga, amesema kuwa mablanketi hayo yana thamani ya Sh laki 9 na kwamba yametolewa wiki iliyopita
Amesema kuwa mablanketi hayo yametolewa kwa raia hao wa kigeni ili yawasaidie kujikinga na baridi wakati wakiwa safarini kurejea katika mataifa yao
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muleba Bw Limbrace Kipuyo, amethibitisha kupokea msaada huo kwa ajili ya raia hao wa kigeni huku akisema kuwa umefika kwa kuchelewa kwa kuwa tayari raia 200 walisharejeshwa makwao


MKUU WA MKOA WA SINGIDA AWATAKA WAKULIMA KUTUNZA ZIADA YA CHAKULA.



 Na;Boniface Mpagape
 Mkuu wa mkoa wa singida Dr parseko Kone amewataka wakulima mkoani humo  kutunza ziada ya chakula kilichopatikana katika mavuno ya msimu huu
Kauli hiyo imetolewa leo katiaka kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa katika ukumbi wa Veta mjini Singida
Dr Kone amestoa kauli hiyo baada ya kusomewa taarifa ya utekelezaji wa sekta  ya kilimo ambayo imeonyesha kuna kuna tani zaidi ya laki nne za ziada katika msimu huu
Taarifa hiyo imesema kuwa bado kuna changamoto ya matumizi ya jembe la la mkono na idara husika inafanbya juhudi za kuelimisha wakulima kutumia teknolojia za kisasa katika kuongeza uzalishaji