Wednesday, January 16, 2013

KERO YA MADAMPO YA TAKA MJINI SINGIDA



Na. Abdul Bandola

Wafanya biashara wa   soko la msufini Mkoani Singida wame ulalamikia ungozi wa Soko hilo kutokujali muda wa kuondoa taka zilizokusanywa na kuwekwa katika maeneo husika(DAMPO) badalayake hujaa na kurudi kuwa uchafu katika maeneo hayo.

 

Hayo yamesemwa na baadhi ya wafanyabiashara wa soko hilo walipokuwa wakizungumza na standard radio sokoni  hapo  kuhusu usafi wa maeneo  hayo ambao wanahofia kupata magonjwaja ya   mlipoko kutokana na kujaa kwa dapo hilo.

 

Hata hivyo mmoja wafanyabiashara hao aliefahamika kwa jina Ramadha Hamza amesema kuwa dampo hilo limekuwa kero kwa baadhi ya wafanya biashara walioko jirani na dampo hilo kitendo kilichopelekea kufunga maduka yao  jambo linalo pelekea bidhaa zao kudhorota na wao kushuka kiuuchumi.

 

Aidha  Bw.Hamza ameuomba uongozi wa soko hilo kushughulikia usafi wa soko hilo mapema iwezakanavyo  ilikuepuka magonjwa ya mlipuko     

 

 

No comments: