Monday, January 14, 2013

JESHI LA POLISI SINGIDA LACHANGIA PATO LA TAIFA


Na. Halima Jamal

JESHI la polisi mkoani Singida limekusanya jumla ya shilingi milioni 487.9 kwa makosa mbalimbali ya usalama barabarani kwa mwaka 2012

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida Linus Sinzumwa ameyasema hayo jana wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa jeshi hilo kwa mwaka 2012 kwa waandishi wa habari na maafisa wa polisi katika sherehe za kuuaga mwaka wa 2012

kamanda Sinzumwa amesema kuwa makusanyo hayo yameongezeka kutoka shilingi milioni 293.5 mwaka 2011 na kuwa ongezeko hilo linaonyesha madereva wamekuwa na mwitikio mdogo wa kuepuka makosa ya usalama barabarani

hata hivyo jeshi la polisi limekiri kuwa kwa sasa madreva wanaokutwa na makosa wamekuwa na mwitikio mzuri wa kutoa faini za makosa wanayokutwa nayo na kujirekebisha.

Aidha  amesema kuwa ajali za barabarani pia zimepungua kutoka ajali 308 kwa mwaka 2011 hadi kufikia ajali 246 mwaka 2012.

Kmebainishwa kuwa watu waliokufa katika ajali hizo kwa mwaka 2011 ni watu 127 na kwa mwaka 2012 waliongezeka na kuwa watu 139, waliojeruhiwa katika ajali hizo ni watu 411 mwaka 2011 na watu 384 kwa mwaka 2012.

Kamanda Sinzumwa alisema kuwa hali ya uhalifu pia imepungua kutoka makosa ya jinai yaliyoripotiwa kwa mwaka 2011kuwa 1404 ukilinganisha na makosa ya jinai yaliyoripotiwa kwa mwaka 2012 kuwa ni 1260 sawa na upungufu wa asilimia 10.

‘’ndugu waandishi kutokana na kupungua kwa uhalifu huo kumewezeshwa kwa asilimia kubwa na wananchi kuitikia wito wa falsafa ya polisi jamii na baadhi ya kata kuanzisha vikundi mbalimbali vya ulinzi shirikishi’’alisema Kamanda Sinzumwa.

Aidha Sinzumwa amewapongeza wandishi wa habari wa mkoa wa Singida kwa kushirikiana kikamilifu katika kutangaza mkoa pamoja na kuwaelimisha wakazi wake juu ya falsafa ya polisi jamii.

No comments: