Sunday, January 6, 2013

RAIS KIKWETE AHIMIZA MAHUBIRI YA AMANI

 
 
NA HALIMA JAMAL

 
Rais kwa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk Jakaya mrisho kikwete amewataka viongozi wa dini kuhubiri amani ya nchi kwenye kila ibada ili kuokoa amani ya nchi inayoyumba kwa sasa.


Kikwete ametoa wito huo jana wakati wa sherehe ya kusimikwa wakfu kwa askofu wa jimbo ya kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania mkoani Singida askofu Dk Alex Seif Mkumbo.


Alisema kuwa miaka ya hivi karibini kumekuwepo na uvunjifu wa amani na vurugu zisizokuwa na maana kutokana na kutofautiana kwa dini na baadhi ya watu kuona dini waliyokuwa nayo wao ni zaidi ya wenzao na kuwa dini ni imani ya mtu.


Aidha Kikwete alisema kuwa viongozi wa dini zote wanawajibu mkubwa kwa kipindi hichi kuokoa taifa kwa kutoa tofauti kati ya dini na dini ila bila kutekeleza wajibu huo tofauti hizo hazitakwisha.


Dk Kikwete alisema kuwa anapata hofu kubwa kwa watu ambao hawana heshima ya kuwasikiliza viongozi wao wa dini na kufuata mambo ya dunia na kuchochea vurugu katika nchi yao wenyewe.


''nawaomba nyie viongozi wa dini mtumie karama mliyopewa na mwenyezi mungu kulinusuru taifa letu lisiangamie kutokana na watu wachache,kwani watu hawa tunaowaongoza ni wetu sote kwa upande wa kiroho ni ninyi viongozi wa dini,na sisi serikali tunaongoza kwa maendeleo ya taifa'',alisema Dk Kikwete.


Kikwete aliwataka viongozi hao kutokata tamaa kuhubiri amani ya nchi kwani binadamu wanaowahubiria wako tofauti.


Sanjari na hilo dk Kikwete amempongeza askofu aliyepewa wakfu huo na kumpa moyo wa kufanya kazi yake aliyopewa na mungu kwa umakini na upendo.


''nakupongeza sana kwa kupewa cheo hicho kwani waliokuchagua wanajua kuwa utawaongoza kwa kufuata miongozo ya mungu na kutangaza dini yako wa watu wote na na kuahidi kushirikiana na mataifa makubwa ya dini ili kuweza kujenga amani ya nchi yetu kwa pamoja tunaweza'',alisema Kikwete.


Kwa upande wake askofu Mkumbo alisema kuwa anamshukuru mungu kwa kumpa wakfu wa kuwatumikia wakristo wa kanisa lake lililoanzishwa mnamo mwaka 1911.


Alisema kuwa amedhamiria kupambana na changamoto zote zinazoikabili amani ya taifa lake na kuhakikisha zinapungua na kumalizika kabisa.


Aidha askofu Mkumbo ameomba ushirikiano kwa watu wote ili wale wote waliokuwa na mpango wa kuvunja amani ya nchi washindwe.


Sherehe hizo zimefanika katika viwanja vya kanisa la KKKT katika manispaa ya Singida na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kidini na serikali.

No comments: