Thursday, January 31, 2013

MAJENGO HAYA YANAPASWA KUTUNZWA KAMA KUMBUKUMBU

JENGO LA ZAMANI LENYE HISTORIA KUBWA YA UKOLONI LINALOTUMIWA NA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRAMBA MKOANI SINGIDA, NI MIONGONI MWA MAJENGO MUHIMU KWA HISTORIA YA TANGANYIKA

HOSPITALI YA RUFAA SINGIDA KUKAMILIKA

Majengo ya Hospitali ya Rufaa nayojengwa mjini Singida, hospitali hii inatarajiwa kusaidia kupunguza tatizo la wagonjwa kusafirishwa kwenda KCMC na Bugando pindi wanapohitaji matibabu ya utaalamu wa juu zaidi

Tuesday, January 29, 2013

DODOMA KUZIMA MITAMBO YA ANALOGIA


Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imekamilisha maandalizi ya kuzima mtambo wa mawasiliano wa analogia na kuwasha mtambo mpya wa digital mkoani  Dodoma.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa utangazaji TCRA Bw. Habi Gunze wakati akizungumza na waandishi wa habari jana ambapo amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya maandalizi ya kuwasha mtambo huo unaotarajiwa kuwashwa usiku wa alhamisi ya wiki hii kukamilika.

Amesema mwezi mmoja sasa umepita tangu jiji la Dar es salaam limehama kutoka mfumo wa analogia na kwenda digitali hivyo kwa sasa ni zamu ya mkoa wa Dodoma na Tanga.

Naye Meneja wa TCRA Bw. Innocent Mungi amewataka wakazi wa mkoani humo kuhakikisha kuwa wamenunua ving’amuzi ili kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza.

Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Dodoma wameipongeza mamlaka husika kwa kufikia hatua hiyo wakati wengine wakilalamikia gharama za matangazo kwani watatakiwa kulipia.   EndS

MABINTI WASHAURIWA KUSUSIA NDOA DHIDI YA VIJANA WASIO NA NYUMBA BORA

Mkuu wa wilaya ya Mkalama Bw. Edward Ole Lenga (kulia) akisisitiza jambo kuhusu ujenzi wa nyumba wilayni humo na kuwataka wavulana wasikimbilie kuoa wakati wakiishi ndani ya Tembe, Tembe ni aina ya mjengo wa asili kwa wakazi wa mikoa ya kati, hususani Singida, Dodoma na sehemu ya miko aya Tabora na Shinyanga.

Serikali wilayani Mkalama mkoani Singida imewataka wasichana kukataa kuolewa na wanaume ambao hawajajenga nyumba za kisasa kama sehemu ya kuhimiza ujenzi wa nyumba bora

Ushauri huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Mkalama Edward ole Lenga wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kwa kipindi cha mwaka 2005 hadi 2012

Bw. Lenga amesema bado wakazi wa wilaya hiyo mpya hawajawa na mwamko wa kujenga nyumba bora na badala yake wanaendelea kuishi katika nyumba za asili maarufu kama tembe

Amesema nyumba hizo za asili si imara na zimekuwa zikihatarisha maisha ya wananchi hasa nyakati za masika
Mkuu huyo wa wilaya amebainisha kuwa serikali licha ya kuhimiza wananchi kujenga nyumba bora bado mwitikio ni mdogo na hivyo kuwaelimisha wasichana na akina mama juu ya umuhimu huo, ndiyo njia pekee ya kuleta mabadililo   

WILAYA YA IRAMBA KUANZISHA CHUO KIKUU


 Mkuu wa wiilaya ya Iramba Bw. Yahaya Nawanda (katikati) akitsoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha mwaka 2005 hadi 2012. Kushoto ni Mbunge wa Iramba Mwigulu Nchemba na kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Bi. Christine Midello.


Serikali kwa kushirikiana na kanisa la kiinjili la kirutheli Tanzania dayosisi ya Kati wameanzisha mchakato wa kujenga chuo kikuu katika mji wa Kiomboi wilayani Iramba

Mkuu wa wilaya ya Iramba Bw. Yahaya nawanda amebainisha hayo jana katika taarifa yake ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005/2012

Ameeleza kuwa kwa mwaka wa masomo wa 2013/2014 chuo hicho kitaanza kudahili wanachuo wa shahada ya kwanza ya ualimu kwa ajili ya chuo kikuu Kiomboi Iramba.

Bw. Nawanda amesema kuanzishwa kwa chuo kikuu mkoani Singida kutasaidia kukuza kiwango cha taaluma kwa shule za msingi na sekondari pamoja na kuongeza uwezekano wa ajira kwa vijana.

MWIGULU NCHEMBA KUWASILISHA HOJA BINAFSI BUNGENI


Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi na naibu katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi Bw. Mwigulu Nchemba anatarajia kuwasiilisha hoja binafsi katika kikao cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma

Akizungumza na Standard Radio Bw. Nchemba ameitaja hoja hiyo kuwa ni kuitaka serikali kuanzisha mfuko maalumu wa elimu ya juu

Amebainisha kuwa Tanzania haina mfuko maalumu wa kuwasaidia vijana wanaojiunga na vyuo vikuu na kwamba fedha zinazotolewa na bodi ya mikopo kwa sasa haina chanzo maalumu na cha uhakika

Kuhusu tabia ya wabunge kugeuza Bunge kama sehemu ya kurushiana maneno na kusababisha vurugu, Bw. Nchemba amesema chama cha mapinduzi kimewaelimisha wabunge wake kupeleka hoja za msingi kwa ustaarabu na kuepuka vurugu
Amesisitiza kuwa Bunge ni mahali pa kwenda kujenga hoja za maendeleo ya wananchi na kwamba chanzo cha vurugu zilizokuwa zikijitokeza mwaka jana Bungeni ni wabunge kuwa na hisia za ubinafsi badala ya kufikiria taifa.

Sunday, January 27, 2013

BODA BODA WAPATA MAFUNZO YA UDEREVA


 
 
 
 
Mkuu wa chuo cha VETA Singida Afridon Mkhomoi, Akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo ya kutunuku vyeti wahitimu wa mafunzo ya udereva wilayani Mkalama.
Picha na Nathanael Limu
 
Serikali  wilayani Mkalama mkoani Singida, imekipongeza chuo cha mafunzo ya ufundi stadi (VETA) Singida, kwa uamuzi wake wa kuanza kuwafuata wateja mahali walipo, badala ya kuwasubiri waje chuoni.

Pongezi hizo zimetolewa na mkuu wilaya hiyo, Bw Edward Ole Lenga wakati akizungumza kwenye halfa ya kufunga mafunzo ya waendesha pikipiki (Bodaboda) iliyofanyika Nduguti, makao makuu ya wilaya mpya ya Mkalama.

Katika hotuba ya Bw. Lenga iliyosomwa kwa niaba yake na mkuu wa kituo cha polisi  Mkalama Bw. Michael Marwa, amesema uamuzi huo wa busara wa kumfuata mteja mahali alipo, una faida nyingi ikiwemo ya kutoathiri shughuli za mteja

Katika hatua nyingine, mkuu huyo wa wilaya, ametoa rai kwa wakazi wote wa wilaya ya Mkalama wanaomiliki na kuendesha pikipiki, magari au vyombo vya moto, kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika kila kata, ili waweze kuletewa mafunzo.
Awali mkuu wa chuo cha VETA Singida Afridon Mkhomoi, amesema mafunzo yanayotolewa na VETA yanalenga kukidhi sera ya nchi ya kuwawezesha vijana kujiajiri na kuwa wajasiriamali.  

245 PEOPLE HAVE DIED IN A FIRE

 Photo By. BBC
 
At least 245 people have died in a fire that swept through a nightclub in a university city in southern Brazil, police and officials say.

Local media say the fire began when a band let off fireworks at the Kiss club in Santa Maria, Rio Grande do Sul.

Reports say panic spread as people tried to get out. Many victims reportedly died from inhaling toxic fumes or from being crushed.

The fire is now out and bodies are being removed from the scene.

President Dilma Rousseff, who cut short a visit to Chile and was returning to Brazil, said everything possible would be done to help the injured and the families of the victims.

I would also like to say to the Brazilian people and to the people of Santa Maria that we stand together at this time, and that even though there's a lot of sadness, we will pull through," she said, speaking from Chile.

In a tweet, the governor of Rio Grande do Sul, Tarso Genro, said it was a "sad Sunday" and that all possible action was being taken in response to the fire. He would be in the city later on Sunday, he added.

NAFASI ZA UWAKALA WA STANDARD RADIO


Tunapenda kukutangazia kuwa, STANDARD RADIO Inatoa fursa kwa wanaohitaji kuwa mawakala wetu katika maeneo mbalimbali kanda ya Kati, mkoa wa SIngida na maeneo ya jirani

kama unapenda kuwa wakala wetu tafadhari leta maombi yako.

By. Utawala

Saturday, January 26, 2013

BIASHARA YA MKAA MKOANI SINGIDA NA MSTAKABALI WA MAZINGIRA


 

WANANCHI mkoani Singida, wameshauriwa kuacha biashara ya uchomaji mkaa, na badala yake waelekeze nguvu zao katika ufugaji wa nyuki, kwa madai kwamba una faida zaidi kuliko biashara ya mkaa.

Wito huo umetolewa juzi na Meneja wakala wa huduma za misitu Tanzania (T.F.S) wilaya ya Singida, Hashimu Kavito, wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mikakati inayochukuliwa na wakala huo, kufanikisha malengo ya upandaji miti, mkoani hapa.

Alisema ufugaji wa nyuki gharama yake ni ndogo mno ukilinganisha na ile ya uchomaji mkaa.

“Pia ufugaji wa nyuki licha ya kuwa hauna gharama kubwa, unayo faida nyingi. Ufugaji wa nyuki unasaidia misitu isikatwe ovyo, bei ya asali na nta, kwa sasa ipo juu mno",alifafanua Hashimu.

Meneja huyo, alisema kutokana na ukweli huo, mfugaji wa nyuki anayo nafasi kubwa ya kuboresha uchumi wake, wilaya, mkoa na hata taifa tofauti na muuza mkaa.

Katika hatua nyingine, aliwataka wananchi wabadilike na kuanza kutambua kuwa miti ni sawa na mazao mengine yaliyozoeleka.

MOHAMED DEWJI AMWAGA MSAADA WA VITENGE SINGIDA


Na. Nathanael Limu

Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Gullam Dewji, ametoa msaada wa pea za vitenge 7,500 zenye thamani ya zaidi ya shilimi 60 milioni, kwa ajili ya kufanikisha maandalizi ya sherehe za CCM kutimiza miaka 36 toka kianzishwe.
Dewji ametoa msaada huo mkubwa na wa aina yake, baada ya kuombwa kufanya hivyo na katibu wa CCm manispaa ya Singida.
Akizungumza na WAANDISHI jana msaidizi wa mbunge Dewji, Duda Mughenyi, alisema jumla ya vikundi vya uhamasihaji 112, vimenufaika na msaada huo wa vitenge.
Alisema pamoja na vikundi hivyo, pia wajumbe wa halmashauri mkuu ya matawi, wafanyabiashara wa kuku za kienyeji soko kuu, boda boda na taasisi mbali mbali, zitanufaika na msaada huo.

“Lengo la kumwomba mbunge Dewji msaada huo wa vitenge, ni kutaka kufanikisha sherehe hizo za chama kikongwe cha CCM kutimiza miaka 36.Chama kuendelea kuwa na mshikamano kwa kipindi chote cha miaka 36, ni jambo la kujivunia na kupigiwa mfano”,alisema Duda.

Msaidizi huyo wa mbunge,alisema kwa hali hiyo, sherehe hii muhimu, ni lazima nayo ipewe heshima ya aina yake ikiwemo wanaccm na wapenzi wake, waonekane tofauti siku hiyo ya sherehe.

Katika hatua nyingine, katibu tawi la Ughaugha (CCM), Hamisi Ramadhani, alisema msaada huo wa vitenge, ni mwendelezo wa misaada mingi ya kimaendeleo anayotoa mbunge Dewji, jimboni kwake.

RAIA WA ETHIOPIA WAHUKUMIWA NCHINI TANZANIA


Na Nathaniel Limu

JUMLA ya raia 12 raia wa nchini Ethiopia,wamehukumiwa na mahakama ya wilaya ya Singida,kulipa faini ya shilingi laki moja (100,000) kila mmoja baada ya kukiri makosa mawili ya kuingia na kuishi ndani ya ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kibali halali.

 

Pia mahakama hiyo,imeamuru basi la kampuni ya Mtei ya mjini Arusha T.797 CDZ lililokuwa limebeba Waethiopia hayo,likamatwe na kutaifishwa kuwa mali ya serikali.

 

Raia hao wa Ethiopia ambao ni bado vijana wadogo na wengine ni wanafunzi wa shule na vyuo, ni pamoja na Ahmed Mohammed Mahamud,Tazana Dijamo Walao, Mohammed Abdi Osman, Abraham Nirato Shango, Adinan Abrahim Abdalah na Alamu Ayele Gabresekesie.

 

Weingine ni Muhidini Sufiani Ahmed, Tasfai Sutatu Kidisu, Yassin Mohammed Hassan, Afandi Aden Suleiman, Ayele Liranso Gafuche na Pakala Agore Mancha.

 

Baada ya nwendesha mashitaka mwanasheria wa serikali Ahmed Seif kuwasomea makosa hayo mawili ya kuingia na kuishini nchini bila ya kuwa na kibali,washitakiwa wote kila mmoja kwa nafasi yake, walikiri kutenda makosa hayo.

 

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo,mwanasheria wa serikali,Seif,aliiomba mahakama hiyo kuwa iwape adhabu kali washitakiwa ikiwa ni njia moja wapo ya kukomesha vitendo vya wahamiaji haramu kuingia na kuishi nchini bila ya kuwa na kibali cho chote halali.

 

"Mheshimiwa hakimu vile vile naiomba mahakama yako itaifishe basi la Mtei lililotumika kuwasafirisha wahamiaji hawa haramu ili kuwaogofya wenye magari kuacha kusafirisha raia wa kigeni wasiokuwa na kibali halali cha kuingia na kuishi nchini"alisema Seif.

 

Akitoa hukumu hiyo, hakimu mfawidhi kiongozi wa mahakama ya wilaya ya Singida, Flora Ndale,alisema mahakama yake imezingatia yale yote yaliyoombwa na upande wa mashitaka na utetesi na kufikia uamuzi wa kutoa adhabu ya kulipa faini ya shilingi laki moja kwa kila mshitakiwa.

 

"Mahakama hii inawatia hatiani na kuwapa adhabu ya kulipa faini hiyo ya shilingi laki moja kila moja na atakayeshindwa kulipa faini,atakwenda kutumikia jela kwa kipindi cha miezi mitatu"alisema hakimu Ndale.

 

Hata hivyo,washitakiwa wote 12,kila mmoja wao alilipa faini hiyo ya shilingi laki moja na hivyo kuachiwa huru.

 

Kwa mujibu wa mwanasheria wa serikali Seif, washitakiwa hao wamekamatwa January 17 mwaka huu alasiri katika eneo la kijiji cha Kititimo nje kidogo ya mji wa Singida wakiwa wametokea mkoani Arusha wakielekea nchini Afrika kusini.

Friday, January 25, 2013

PARACHUTI KUTUMIKA MLIMA KILIMANJARO


Wakazi waishio jirani na mlima Kilimanjaro watanufaika na utalii wa kuruka milima kwa maparachuti utakaofanyika kwa mara ya kwanza nchini, mwezi februari mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari, afisa habari wa mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanapa Bw. Pascal Shelitete amesema fedha zitakazopatikana kupitia utalii huo zitabaki nchini na wananchi waishio jirani na mlima Kilimanjaro watanufaika kupitia mradi wa utunzaji mazingira.

Mradi huo ni pamoja na shughuli zinazohusu masuala ya virusi vya ukimwi, mradi wa maji safi na salama chini ya asasi za one foundation, water International, na plant purpose.

Tukio hilo linatarajiwa kukusanya zaidi ya watalii mia moja kutoka nchi ishirini na tano duniani, na imelenga kukusanya takribani shilingi bilioni mbili za Kitanzania.

 

POLISI WAJENGEWA NYUMBA IRAMBA


Mkuu wa jeshi la Polisi mkoani SIngida ACP Linus Sinzumwa (katikati) akikagua ujenzi wa nyumba ya kuishi askari katika kituo cha polisi Misigiri wilayani Iramba , Ujenzi huo unatekelezwa na wananchi wa kata ya Misigiri ambao wameamua kufanya hivyo baada ya kukerwa na uharifu na kisingizio cha polisi kutokuwa na makazi.

MANSPAA YA SINGIDA YALAUMIWA KUTWAA ARDHI YA WANANCHI


Wakazi wa vitongoji vya Mwamtanda na Mwaja kata ya Mandewa wameilalamikia halmashauri ya Manispaa  ya Singida  kwa kutotimiza ahadi ya kuwalipa fidia waliyoitoa wakati  maeneo yao  ya  ardhi  yalipochukuliwa na serikali  kwa ajili ya upimaji wa viwanja vipya.

Wakazi hao wamesema hayo jana wakati  wakizungumza na Mkuu wa wilaya ya Singida  Bi. Queen Mlozi, baada ya kutembelea vitongoji hivyo.

Wakazi hao wamesema,  wakati serikali inahitaji viwanja  waliahidiwa kuwa kila mtu  atapewa kiwanja na kulipwa fidia jambo ambalo halikutekelezwa, hali  iliyopelekea baadhi ya wananchi kukosa makazi.

Wamesema  baadhi yao wamekwenda  katika ofisi za ardhi ili  kutaka kupata maelekezo zaidi na kuonyeshwa sehemu  mbadala na kufuatilia fidia  zao, badala yake  wamepewa  barua za kutakiwa kuondoka katika maeneo yao.

Mkuu wa  wilaya  ya Singida  Bi.  Mlozi  amewataka wakazi hao kuwa na subira kwa kuwa suala hilo linatafutiwa ufumbuzi.

WANAJESHI WA RWANDA WATEKWA KAGERA


Wanajeshi wa jeshi la Rwanda waliokuwa wakisafiri kutoka Kigari kwenda Dar es Salaam wamenusurika kifo baada ya watu wanaotajwa kuwa majambazi kuliteka gari walimokuwa wakisafiria


Tukio hilo limetokea alfajiri leo majira ya saa 12:45 asubuhi katika kijiji cha KIkoma Kata ya Lusahunga wilayani biharamulo moani Kagera


Katika tukio hilo jumla ya magari matano yametekwa na watu wenye silaha nzito za kivita


Akizungumuza Standard Radio kwa njia ya simu Diwani wa kata ya Lusahunga Bw. Amoni Mizengo amesema, wanajeshi hao wa Rwanda walikuwa wakisafiri kwenda Dar es salaam kununua magari.


Aidha askari mmoja wa jeshi la polisi Tanzania Kituo Cha Nyakahura wilayani Biharamlo ni miongoni mwa waliotekwa na kuporwa vitu mbalimbali


Mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Kagera ACP Phillip Kallang amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi                                        ENDS

KATIBA IWATAMBUE WALEMAVU WA NGOZI


Wajumbe wa kamati ya chama cha albino mkoa wa singida TAS, wamefanya semina ya mafunzo ya siku mbili katika ukumbi wa kituo cha walimu nyerere katika manispaa ya Singida yakuwawezesha kutambua haki zao na kutoa maoni kuhusu katiba wanayoitaka.

Akitoa mafunzo hayo Bw. Godwel Mwamakula ambae ni  mwanasheria ofisi ya kazi kwa mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa singida amesema kuwa walemavu wa ngozi ni lazima watambue haki zao za msingi, ili waweze kutoa maoni yao katika katiba itakayoundwa.

Bw. Mwamakula ameongeza kuwa katiba iliyopo haijaweka wazi haki anazohitaji kupata mlemavu wa ngozi hivyo katiba ijayo lazima iundwe tume itakayochunguza na  kuhakikisha viongozi wote wanatambua mahitaji ya makundi maalum wanakuwa waadilifu na mahakama ipewe uhuru wa kusikiliza madai ya haki za walemavu hao.

Akihitimisha semina hiyo, Bw Mwamakula amesema kuwa ulinzi shirikishi na polisi jamii ni kwa ajili ya usalama wa raia na mali zao,  hivyo watumie fursa hiyo kutoa taarifa wakiwa na tatizo lolote ili kuondokana na vitendo vya unyanyasaji katika maeneo wanayoishi na  kufikisha waliyopata kwenye semina kwa wenzao.

Kwa upande wao walemavu wa ngozi wamesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile, ukosefu wa mafuta ya kulainisha ngozi zao, gharama za elimu, matibabu na kufanya kazi ngumu. Wameiomba serikali kupitia katiba itakayoundwa kuangalia changamoto hizo.

WAPANGAJI WA NYUMBA MKOANI SINGIDA WALALAMA


Baadhi ya wapangaji katika manispaa ya  singida wamelalamikia wenye nyumba kwa kuwanyanyasa na kuwadharau kwani na wao wanahitaji kuheshimiwa.ili waweze kuishi kwa huru kama watu wengine.

 

Hayo yamesemwa na mmoja wa wapangaji Bi.Rehema mussa alipozungumza na standard radio ambapo amesema kuwa wenye nyumba wamekuwa wakiwadharau wapangaji kwa kuwatolea kauli chafu, kitendo kinachowafanya  waishi bila amani na kuwa na hofu wakati wote.

 

Naye Bw. Haruna Issa amesema kuwa wenye nyumba ni lazima watambue kuwa wapangaji wanahitaji kuthaminiwa kwani wengi wao walikotoka wana nyumba pengine nzuri kuliko hata hizo.

 

Hata hivyo ameongeza kwa kusema kuwa wenye nyumba lazima wawe na msimamo katika  mapatano ili kuepusha usumbufu unaojitokeza kutokana na baadhi yao kubadilisha kodi kinyume na maelewano baina yao na wapangaji.

 

TANGAZO MAALUM KUTOKA STANDARD VOICE LTD


Tunapenda kukutangazia kuwa kituo chetu cha Radio kiitwacho STANDARD RADIO FM sasa kimeanza kurusha matangazo yake mkoani Singida

 

Miongoni mwa matangazo yanayorushwa na Radio hii ni Taarifa za habari, Vipindi mbalimbali pamoja na burundani ya Muziki mchanganyiko wenye ladha inayoendana na mahitaji ya msikilizaji

 

Aidha vipindi vyetu pia vinaandaliwa na watayarishaji mahili kwa kuzingatia uhitaji wa jamii, kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni

 

Miongoni mwa vipindi tulivyonavyo ni

·       HOJA YA LEO

·       UCHUMI WETU

·       UKULIMA NA MAZINGIRA NA UFUGAJI

·       UKIMWI

·       ELIMU YETU

·       HAKI NA USAWA

·       ULIMWENGU WA MICHEZO

·       UJASIRIAMALI

·       WATOTO

·       VIJANA NA UJANA

·       UZEE NI TUNU

·       WAJIBU WAKO

·       AFYA NA UZAZI

 

Standard radio inasikika katika masafa ya FM - 90.10 MHz na inasikika mkoa mzima wa Singida pamoja na maeneo yafuatayo

 

1.   Igunga

2.   Nzega

3.   Uyui

4.   Kondoa

5.   Katesh

6.   Mbulu

7.   Manyara

8.   Bahi

9.   Hanang

na maeneo mengine jirani na mkoa wa Singida

Tunakukaribisha kuitegea sikio Radio Yako STANDARD RADIO FM Sauti ya Wasiosikika na tunakukaribisha ulete habari, matangazo, maoni na maswali pia
 
Aidha tunao wawakilishi wetu kutoka mikoa ifuatayo KIGOMA, DODOMA, RUKWA, KAGERA, MANYARA na DAR ES SALAAM

 
Ukiwa na Tangazo, taarifa, hoja yoyote tafadhari wasiliana nasi kwa anuani ifuatayo

 

SLP 62 SINGIDA

SIMU. 0786200518, 0787 592056, 0764243377

BARUA PEPE srfm2011@gmail.com

Tupo pia katika mitandao ya jamii TWITTER na FACEBOOK

Waweza pia kututembelea katika BLOG yetu kwa anuani ifuatayo www.standardradiofm.blogspot.com

 

STANDARD RADIO FM, SAUTI YA WASIOSIKIKA

Wednesday, January 23, 2013

WATU WATATU WAFARIKI DUNI MKOANI KIGOMA


Na. Mwandishi wetu
 

Jeshi la polisi Mkoani Kigoma limebainisha kuwepo kwa Watu watatu wambao amefariki dunia katika matukio mawili tofauti wilayani kasulu mkoani Kigoma kati ya Januari 21 na 22 mwaka huu likiwemo tukio la mtu kujinyonga.

 

Kamanda wa polisi mkoani Kigoma ACP Frasser Kashai amebainisha hayo leo na kutaja kuwa katika tukio la kwanza mtoto wa umri wa miaka 15, Sharifu Rajabu mkazi wa kijiji cha Nyarugusu wilayani Kasulu alikutwa amejinyonga nyumbani chumbani kwake nyumbani kwao kwa kutumia kamba ya chandarua.

 
Imeelezwa kuwa, tukio hilo limetokea Januari 21 majira ya saa nne kamili asubuhi katika kitongoji cha Chiloziye, kijiji cha Nyarugusu,kata ya Makere wilayani humo na kwamba sababu za kujinyonga bado hazijafahamika huku upelelezi zaidi juu ya tukio hilo ukiendelea.

 

Aidha katika tukio lingine kamanda Kashai amesema wakazi wawili wa kijiji cha Kwaga wilayani Kasulu Bw. Paulo Hakani mwenye umri wa miaka 45 na bi.Prisca William mwenye umri wa miaka 23 wamefariki dunia baada ya kupigwa na radi wakiwa shambani kwao Januari 22 mwaka huu kufuatia mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.

EndS

POLISI KUYAFUNGA MAKAMPUNI YA ULINZI TABORA

Na. Moses mabula

KAMANDA wa Polisi mkoani Tabora ACP Anthony Rutta amesema kuwa atayafungia kufanyakazi makampuni yote ya ulinzi mkoani humo ambayo yanashindwa kutekeleza masharti yaliyopewa na jeshi hilo.

 

Mkuu huyo wa Polisi mkoa wa Tabora amesema kwamba jeshi la Polisi lilitoa masharti kwa wamiliki wa makampuni yaho kuwa hayaruhusiwi kuajiri walinzi wasio waadilifu ambao wamekuwa wakila njama za kufanya uharifu wa wizi kwenye taasisi mbalimbali ambayo wameingia nazo mkataba wa ulinzi.

 

Akizungumza na mwandishi wa habari ofisini kamanda Ruta alikiri kuwepo kwa baadhi ya makampuni ya ulinzi ambayo hayafuati taratibu za ajira za walinzi huku akiapa kuyashughulikia ipasavyo kwakuwa baadhi ya makampuni hayo yamekuwa yakiajiri walinzi wasio na sifa na kukosa uaminifu.

 

Kuhusu matukio ya hivi karibuni ya wizi uliofanyika katika Shirika lisilo la kiserikali la Total Land care ambalo lilipata hasara ya zaidi ya shilingi mil.kumi na tatu baada ya walinzi wa kampuni ya ulinzi ya Alliance Day & Night la hapa mjini Tabora ambao wanadaiwa kula njama na kufanya wizi wa kuvunja ofisi za Shirika hilo.

 

Kamanda Rutta amesema bado Polisi wanaendelea na uchunguzi lakini mlinzi mmoja wa kampuni hiyo anayefahamika kwa jina la Said Kayungilo alitoweka kabla ya kukamatwa.

Monday, January 21, 2013

KITUO CHA MABASI UBUNGO CHALETA BALAA


Watu watatu wamejeruhiwa  na magari ishirini na manne kuharibika baada ya ukuta wa kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar es salaam  kuanguka leo asubuhi katika eneo la kuegeshea magari.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Kenyela amesema ukuta hbuo umeanguka kufuatia kazi ya ubomoaji inayoendelea katika eneo hilo. Amesema watu waliojeruhiwa wamepelekwa hospitali kupata matibabu.
Kufuatia ajali hiyo watu wametakiwa kuwa waangalifu katika eneo la kituo cha mabasi Ubungo, ili kuepuka athari zinazoweza kutokea wakati zoezi la kuondoa magari yaliyoangukiwa na ukuta, likifanyika

KANISA LA ANGLIKANA LAKIRI KUKABILIWA NA UKATA



Waumini wa kanisa la Anglikana mjini Singida leo wamekumbushwa  kuwa kutoa sadaka ni sehemu ya ibada.

 

Akihubiri katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Paulo, mwinjilisti Musa Njagamba amesema awali kanisa hilo lilitegemea misaada kutoka kwa wafadhili hivyo waumini wanapaswa kujenga tabia ya kutokuwa tegemezi bali wanapaswa kujitolea ili kuliendeleza kanisa lao.

 

Amesema neno la Mungu halihitaji msaada kutoka nje bali waumini wanapaswa kubadili mienendo kwa kutoa sadaka ili kanisa hilo liweze kujiendesha lenyewe.

CHADEMA WAWALALAMIKIA WANAWAKE


Mratibu wa sera za chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoani Singida Bi Jesca Kishuwa amelalamikia baadhi ya   wanawake mkoani Singida kutohudhuria  katika mikutano ya hadhara  hasa ya kisiasa.

 

Bi Jesca amesema hayo jana wakati wa mkutano wa hadhara wa  chama cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA) uliofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani ya mabasi mkoani Singida.

 

Bi Jesca ameeleza kuwa licha ya idadi kubwa ya watanzania kuwa na kundi kubwa la wanawake, bado akina mama wako nyuma kimaendeleo na kiufahamu kutokana na kutojihusisha na masuaala ya kisiasa

MKUU WA MKOA WA SINGIDA ACHACHAMAA


Mkuu wa mkoa wa Singida Dr, Parseko Kone ameonya tabia ya baadhi ya maafisa wa serikali na vyombo vya habari kutoa taarifa zisizo sahihi kwa wananchi
 
Dr. Kone amesema hayo jana katika hafla fupi ya kuuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013, iliyofanyika katika chuo cha utumishi wa Umma mjini Singida
 
Dr. Kone amesema hayo kufuatia vyombo vya habari kuripoti habari ya uhaba wa chakula mkoani Singida, na kutaja kuwa takwimu zilizotolewa katika habari iliyochapishwa na moja ya magazeti ya kil asiku si sahihi
 
Mwishoni mwa wiki, baraza la madiwani wilaya ya Singida lilikiri kuwepo kwa uhaba mkubwa wa chakula na kuagiza uongozi wa halmashauri hiyo kulitafutaia ufumbuzi mara moja
 

Friday, January 18, 2013

POLISI SINGIDA WAPATA PIKIPIKI KUIMARISHA ULINZI


 
 
 
 
 
 
 
 
ACP Linus Sinzumwa Kamanda wa polisi mkoa wa Singida
 
 
 
 
Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema ametoa jumla ya piki piki 22 kwa jeshi la polisi mkoani Singida, kama sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kuimarisha ulinzi nchini na kusogeza huduma za usalama jirani na wananchi

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Linus Sinzumwa amebainisha kuwa pikipiki hizo zitasambazwa katika tarafa za mkoa huo

Kamanda Sinzumwa amebainisha kuwa piki piki hizo zitakabidhiwa kwa askari wateule ambao watazitumia kwa ajili ya kufanya doria na kuzuia uharifu katika tarafa ambazo watapangiwa pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya raia na jeshi hilo

Mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone, anatarajiwa kukabidhi vyombo hivyo vya usafiri kwa jeshi hilo mapema wiki ijayo

MKUU WA MKOA SINGIDA ATOA AGIZO KWA WAKUU WA WILAYA


Wakuu wa wilaya zote mkoani Singida wameagizwa kuwajulisha wananchi juu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi tangu mwaka 2005 hadi mwaka 2012, kupitia vyombo vya habari vinavyowafikia wananchi kwa urahisi.

Agizo hilo limetolewa hivi karibuni na Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Ole Kone, wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa waandishi wa habari ofisini kwake.
 
Dk. Kone amesema wakuu wa wilaya wakifanya hivyo na wananchi kupewa fursa ya kutoa maoni yao, itakuwa ni njia rahisi kufikisha taarifa kwa wananchi ambao nao watatoa maoni yao moja kwa moja na kuhoji wataalam wa sekta mbali mbali juu ya utekelezaji wa ilani hiyo.

Wakuu wa wilaya zote mkoani Singida wameahidi kutoa taarifa za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika wilaya zao kutumia vyaombo vya habari.