Pichani: Ndg. Prosper kwigize, Mratibu mradi wa Standard Radio fm, iliyopo Mjini Singida nchini Tanzania.
Mratibu wa maradi wa Standard Radio iliyopo mjini
Singida Bw. Prosper Kwigize ametoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Singida na mikoa
jirani inakosikika redio hii, kuitumia ipasavyo kwa kushiriki kikamilifu katika
kuandaa vipindi mbali mbali na kutoa
maoni yao na kupitia chombo hiki cha habari.
Bw. Kwigize ametoa wito huo jana, wakati
akiutangazia umma kuwa sasa Standard redio imeanza rasmi kutangaza habari
pamoja na vipindi ambavyo vitalenga
sekta mbali mbali katika jamii.
Amesema endapo wakazi wa mkoa wa Singida watakitumia
ipasavyo chombo hiki cha habari watajiletea maendeleo pamoja na kutafuta
ufumbuzi wa martatizo yanayowakabili kwani mawasiliano ni nyanja muhimu katika
jamii.
1 comment:
Hongera sana wajina,juhudi zako tunaziona na tunazidhamini sana.
Post a Comment