Mamlaka ya mawasiliano
Tanzania TCRA imekamilisha maandalizi ya kuzima mtambo wa mawasiliano wa
analogia na kuwasha mtambo mpya wa digital mkoani Dodoma.
Hayo yamesemwa na
Mkurugenzi wa utangazaji TCRA Bw. Habi Gunze wakati akizungumza na waandishi wa
habari jana ambapo amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya maandalizi ya
kuwasha mtambo huo unaotarajiwa kuwashwa usiku wa alhamisi ya wiki hii
kukamilika.
Amesema mwezi mmoja
sasa umepita tangu jiji la Dar es salaam limehama kutoka mfumo wa analogia na
kwenda digitali hivyo kwa sasa ni zamu ya mkoa wa Dodoma na Tanga.
Naye Meneja wa TCRA Bw.
Innocent Mungi amewataka wakazi wa mkoani humo kuhakikisha kuwa wamenunua
ving’amuzi ili kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza.
Baadhi ya wakazi wa
mkoa wa Dodoma wameipongeza mamlaka husika kwa kufikia hatua hiyo wakati
wengine wakilalamikia gharama za matangazo kwani watatakiwa kulipia. EndS
1 comment:
Habari za majukumu,
Pia poleni na kazi,na hongereni kwa usikivu mzuri wa Matangazo yenu
Post a Comment