Waumini wa kanisa la Anglikana mjini
Singida leo wamekumbushwa kuwa kutoa
sadaka ni sehemu ya ibada.
Akihubiri katika kanisa la Anglikana
la Mtakatifu Paulo, mwinjilisti Musa Njagamba amesema awali kanisa hilo
lilitegemea misaada kutoka kwa wafadhili hivyo waumini wanapaswa kujenga tabia
ya kutokuwa tegemezi bali wanapaswa kujitolea ili kuliendeleza kanisa lao.
Amesema neno la Mungu halihitaji
msaada kutoka nje bali waumini wanapaswa kubadili mienendo kwa kutoa sadaka ili
kanisa hilo liweze kujiendesha lenyewe.
1 comment:
Nadhani waumini wanapaswa watambuwe kuwa ni juhudi zao pekee zitakazisaidia kuondoa ukata unalikabili kanisa lao.Kwa hiyo ni vema wakajipanga.
Wajia
Dsm.
Post a Comment