WANANCHI mkoani Singida, wameshauriwa kuacha
biashara ya uchomaji mkaa, na badala yake waelekeze nguvu zao katika ufugaji
wa nyuki, kwa madai kwamba una faida zaidi kuliko biashara ya mkaa.
|
Wito huo umetolewa juzi na Meneja wakala wa huduma za
misitu Tanzania (T.F.S) wilaya ya Singida, Hashimu Kavito, wakati akizungumza
na waandishi wa habari juu ya mikakati inayochukuliwa na wakala huo,
kufanikisha malengo ya upandaji miti, mkoani hapa.
Alisema ufugaji wa nyuki gharama yake ni ndogo mno
ukilinganisha na ile ya uchomaji mkaa.
“Pia ufugaji wa nyuki licha ya kuwa hauna gharama
kubwa, unayo faida nyingi. Ufugaji wa nyuki unasaidia misitu isikatwe ovyo, bei
ya asali na nta, kwa sasa ipo juu mno",alifafanua Hashimu.
Meneja huyo, alisema kutokana na ukweli huo, mfugaji
wa nyuki anayo nafasi kubwa ya kuboresha uchumi wake, wilaya, mkoa na hata
taifa tofauti na muuza mkaa.
Katika hatua nyingine, aliwataka wananchi wabadilike
na kuanza kutambua kuwa miti ni sawa na mazao mengine yaliyozoeleka.
No comments:
Post a Comment