Na. Abdul Bandola
Wafanya biashara wa
soko la msufini Mkoani Singida wame ulalamikia ungozi wa Soko hilo
kutokujali muda wa kuondoa taka zilizokusanywa na kuwekwa katika maeneo husika(DAMPO)
badalayake hujaa na kurudi kuwa uchafu katika maeneo hayo.
Hayo yamesemwa na baadhi ya wafanyabiashara wa soko hilo
walipokuwa wakizungumza na standard radio sokoni hapo
kuhusu usafi wa maeneo hayo ambao
wanahofia kupata magonjwaja ya mlipoko kutokana na kujaa kwa dapo hilo.
Hata hivyo mmoja wafanyabiashara hao aliefahamika kwa jina
Ramadha Hamza amesema kuwa dampo hilo limekuwa
kero kwa baadhi ya wafanya biashara walioko jirani na dampo hilo
kitendo kilichopelekea kufunga maduka yao jambo linalo pelekea bidhaa zao kudhorota na
wao kushuka kiuuchumi.
Aidha Bw.Hamza
ameuomba uongozi wa soko hilo kushughulikia usafi wa soko hilo mapema
iwezakanavyo ilikuepuka magonjwa ya
mlipuko
No comments:
Post a Comment