Picha kutoka maktaba SR FM
By. Deborah Marco na Neema Jullius
Jumla ya vyandarua 86,804 zimegawiwa kwa akina mama wajawazito mkoani Singida katika kipindi cha mwaka 2012 kwa lengo la kuhakikisha akina mama na watoto wanakingwa na maralia na kupunguza vifo vya wajawazito na watoto chini ya miaka mitano
Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi, wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kwa kipindi cha mwaka 2002 hadi 2012
Mwalimu Mlozi amebainisha kuwa katika kipindi cha mwaka 2005 viligawiwa vyandarua 66506 tofauti na mwaka 2012 sawa na asilimia 30.5 na kwamba ongezeko hilo limetokana na elimu inayotolewa sambamba na mkakayi wa kukomesha vifo vya wajawazito na watoto
Taarifa hiyo ya mkuu wa wilaya ya Singida ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya mkuu wa Mkoa wa Singida Dr. Paraseko Kone ambaye ameagiza kila mkuu wa wilaya kutoa taarifa kwa wananchi na wadau wa maendeleo juu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha mwaka 2005-2012
No comments:
Post a Comment