Chuo cha Uhasibu TIA Singida eo kimeingia katika mgogoroo wa
utawala na wanachuo kufuatia uwepo kwa dosari katika uchaguzi wa viongozi wa
wananchuo halii iliyopelekea jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia na
vyombo vingine vya usalama kukizingira chuo hicho
Imeelezwa kuwa wanachuo hao wameamua kufanya vurugu dhidi ya
uongozi baadaya aliyetangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya rais wa serikali ya
wanachuo kutokuwa na sifa za ushindi kwa mujbu wa kanuni za uchaguzi wa
serikali za wachachuo Tanzania
Standard Radio imeshuhudia kundi kubwa la askari polisi
wenye silaha za moto na mabomu ya machozi wakiwa wametanda eneo zima la chuo
hicho hicho,
Aidha wanachuo wanaonekana kukaa katika makundi makundi
wakijadili na kulalamikia ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment