Abdul Bandola na Edilitruda Chami
Watu watatu wa familia moja
wamefariki dunia katika kijiji cha Itigi wilaya ya Manyoni Mkoani Singida baada
ya kula uyoga unaosadiki kuwa na sumu.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya
habari kamanda wa polisi mkoa wa Singida ACP Linusi Sinzumwa amesema tukio hilo limetokea tarehe 15 Januari 2013.
Amesema mwanamke mmoja ambaye
ametambuliwa kwa jina la Agnes Muna mwenye umri wa miaka 19 alipika uyoga aliouchuma shambani mwake kwa ajili ya kitoweo
na kwa cha famillia pasipo kujua kama una sumu.
Kamanda Sinzumwa amesema baada ya
muda mfupi watoto walianza kutapika na kuishiwa nguvu ndipo walipopelekwa
katika hospitali ya wilaya ya Manyoni kupatiwa matibabu lakini walifariki
dunia.
Amewataja waliokufa kuwa ni Yese Jeremia mwenye umri wa miaka 6, Joshua Jeremia
mwenye umri wa miaka 3 pamoja na mama yao Agnes Muna aliyefariki baadaye
No comments:
Post a Comment