Friday, January 4, 2013
RAIS KIKWETE KUZURU SINGIDA KESHO
Rais Jakaya Kikwete anafanya ziara ya siku mbili mkoani Singida ambapo pamoja na mambo mengine atashiriki ibada ya kumweka wakifu Askaofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri KKKT Dayosisi ya Kati Dr. Alex Seif Mkumbo
Mkuu wa mkoa wa Singida ametoa taarifa hiyo leo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari mjini Singida, na kuongeza kuwa Rais Kikwete baada ya kumaliza kushiriki ibada hiyo January 6, 2013 atasafiri kuelekea mkoani Tabora kuendelea na ziara yake.
Kikwete atapokelewa wilayani Manyoni kabla ya kuwasili mjini Singida siku ya jumamosi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment