Chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania {TASWA} kisiwani Zanzibar kimeunda timu ya soka
itakayojumuisha waandishi wa habari za michezo na burudani
Akizungumza na waandishi wa habari katibu wa chama hicho
Donisya Thomas amasema kuwa wachezaji wa timu hiyo watakuwa wale waliojiunga na
chama hicho tuu,na kwamba madhumuni ya kuunda timu hiyo ni kudhihirisha kwa vitendo
kuwa waandishi wa habari na wao ni wanamichezo hodari na siyo waandishi wa habari za michezo pekee
Aidha amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kuwapa furksa zaidi
wanamichezo ya kuweza kuwa na afya njema ya wanachama wao na kwamba wanataswa watatambulika kitaifa na kimataifa
Pamoja na hayo katibu huyo amesema kuna changamoto
zinazowakabili kama vile ukosefu wa vifaa vya
kufanyia mazoezi,jezi na mahitaji mengine yanayohitajika wakati wa michezo
Timu hiyo kwa sasa itakuwa chini ya kocha wake Ali Bakari
Cheupe,ambapo katibu ni Ameir Khalid, mwekahazina ni mwajuma juma,mwenyekiti ni
mwinyimvua Abdi Mzukwi
No comments:
Post a Comment