Na Edilitruda Chami
Wito umetolewa kwa waandishi wa habari mkoani Singida kutumia
kalamu zao vizuri na kuepuka uchochezi katika taarifa mbalimbali ili kujenga
nchi kwa amani na utulivu
Wito huo umetolewaa ma kamanda wa mkoa wa Singida A.C.P
Linus Sinzumwa katika tafrija ya jeshi la polisi na waandishi wa habari
iliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Singida
Amesema ni vyema habari zinazopatikana za kiuhalifu ama za
kisiasa zikafanyiwa uchambuzi yakinifu kabla ya kutangazawa au kuchapishwa
Amesisitiza kuwa waandishi ni kichecheo cha maendeleo na kwamba
habari zinaweza kujenga au kubomoa amani ya nchi pale kalamu zao zinapotumika kinyume
Aidha amezitaja nchi za Misri na Libya kama mifano ya nchi
za afrika ambazo serikali zao zimepinduliwa kwa kupitia nyanja za mawasiliano
ya habari na kwamba waandishi wasisite kutoa taarifa katika vituo vya polisi
pale wanapopata vitisho vya namna yoyote
ili hatua zichukuliwe mara moja
No comments:
Post a Comment