Wednesday, January 23, 2013

WATU WATATU WAFARIKI DUNI MKOANI KIGOMA


Na. Mwandishi wetu
 

Jeshi la polisi Mkoani Kigoma limebainisha kuwepo kwa Watu watatu wambao amefariki dunia katika matukio mawili tofauti wilayani kasulu mkoani Kigoma kati ya Januari 21 na 22 mwaka huu likiwemo tukio la mtu kujinyonga.

 

Kamanda wa polisi mkoani Kigoma ACP Frasser Kashai amebainisha hayo leo na kutaja kuwa katika tukio la kwanza mtoto wa umri wa miaka 15, Sharifu Rajabu mkazi wa kijiji cha Nyarugusu wilayani Kasulu alikutwa amejinyonga nyumbani chumbani kwake nyumbani kwao kwa kutumia kamba ya chandarua.

 
Imeelezwa kuwa, tukio hilo limetokea Januari 21 majira ya saa nne kamili asubuhi katika kitongoji cha Chiloziye, kijiji cha Nyarugusu,kata ya Makere wilayani humo na kwamba sababu za kujinyonga bado hazijafahamika huku upelelezi zaidi juu ya tukio hilo ukiendelea.

 

Aidha katika tukio lingine kamanda Kashai amesema wakazi wawili wa kijiji cha Kwaga wilayani Kasulu Bw. Paulo Hakani mwenye umri wa miaka 45 na bi.Prisca William mwenye umri wa miaka 23 wamefariki dunia baada ya kupigwa na radi wakiwa shambani kwao Januari 22 mwaka huu kufuatia mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.

EndS

No comments: