NA. Halma Jamal
MPANGO wa kilimo
(DADPS), halmashauri za Wilaya za Mkoa wa Singida, umechimba malambo sabini,
ikilinganishwa na 19 yaliyokuwepo miaka saba iliyopita, kuwezesha mifugo kupata
maji.
Malambo hayo
yamechimbwa kwa ushirikiano kati ya serikali kuu, halmashauri na wananchi kati
ya mwaka 2005 hadi 2012.
Mkuu wa mkoa, Dk.
Parseko Kone, alisema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake,
juu ya utekelezaji wa ilani ya CCM mkoa wa Singida, kwa kipindi cha miaka saba
iliyopita.
Dk. Kone alisema
katika kipindi hicho, kumekuwa na ongezeko la la madume bora ya
ng’ombe kutoka 88 mwaka 2005 hadi kufikia 608 mwaka jana.
Alisema mpango wa
uhamilishaji mifugo ya asili ulioanza mwaka 2008/2009 umeonyesha mafanikio kwa
kuongeza idadi ya ng’ombe waliohamilishwa hadi kufikia 1,267, huku ndama wakiwa
672 hadi kufikia mwaka 2012.
Dk. Kone alisema
katika kipindi hicho elimu kupitia mifugo darasa imeongezeka kutoka wafugaji 327
hadi kufikia wafugaji 7,561, hali ambayo pia imeongeza takwimu za wafugaji bora
na idadi ya ng’ombe walioboreshwa.
Aidha Dk. Kone alisema
mwaka 2005 hapakuwa na kiwanda cha kusindika bidhaa za ngozi na maziwa lakini
hadi mwaka jana kuna viwanda vidogo vinne vinavyotengeneza bidhaa zitokanazo na
mazao ya ngozi.
Alisema pia wafugaji
kuku wa kienyeji wa biashara wenye kufuga kuanzia kuku 100, watu 503 walipatiwa
mafunzo hadi kufikia 2010/2011, wakiwa na kuku 50,300, ikilinganishwa na
wafugaji saba mwaka 2006/2007.
Mkoa wa Singida una
jumla ya mifugo mbalimbali ikiwemo mbuzi, ng'ombe na kondoo 4,145,819, huku kuku
pekee wakiwa ni 1,730,031.
No comments:
Post a Comment