Mkuu wa Mkoa Singida Dakta Paserko Kone ametangaza kuwa ataunda tume ya kufanya uchunguzi wa chanzo cha moto uliounguza nyumba ya shirika la nyumba la taifa na kusababisha hasara kubwa kwa wapangaji waliokuwa na maduka na makazi katika nyumba hiyo
Mkuu huyo wa mkoa amefikia azima hiyo baada ya kukosa habari sahihi za chanzo cha moto huo pamooja na kutaarifiwa kuwa kikosi cha zima moto mkoani Singida kimeshindwa kufika kwa wakati kuuzima moto huo kwa visingizio mbalimbali ikiwemo kukosa maji na uchakavu wa matari ya gari la kuzima moto
Mmoja wa wapangaji waliokuwa wanaishi na kufanya biashara
ndani ya Nyumba hiyo ni pamoja na Bi Aida Mlei ambaye alifanikiwa kumwokoa
mwanae mwenye umri wa miaka mitano amesema kuwa yeye hajui nini hasa chanzo cha
moto huo kwani mwanae huyo ndiye alikuwa anaangalia runigna sebuleni ambako
kulikuwa na makochi, jiko la umeme na gesi, kabati la vyombo, magunia ya mchele
ambavyo vimeteketea vyote
Kwa mujibu wa jirani wa nyumba hiyo Bwana Saduni Halfani
amesema kuwa zima moto zilizotumika zimetoka majumbani kwao kwani gari la zima
moto lilishindwa kutoa huduma hiyo kwa kuwa na matatizo yaliyosemekana kuwa ni
ya kiufundi
hili ni tukio la pili kwa nyumba ya biashara kuungua moto mjini singida katika eneo la soko kuu, na lawama zote kupelekwa kwa kikosi cha zima moto
Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha kuzima moto Bwana
Kelvin Mapunda amekiri kuwa gari la zima moto lilikuwa na matatizo ya matairi
hatimaye kushindwa kutoa msaada wakati wa ajali hiyo
huyu ni mmoja wa wananchi ambaye alijitosa ndani ya nyumba hiyo kujaribu kuokoa uhai wa binadamu, hata hivyo alipata majeraha na kupata huduma ya kwanza.
Taarifa za awali zinaonesha kuwa, hakuna kifo kilichotokea na thamaniya mali zilizoharibiwa haijafahamika.
Standard Radio Itaendelea kufuatilia na kuendelea kukuletea taarifa zaidi
Habari hii imeandaliwa na EUFRASIA MATHIAS, SAADA SALUM MASOUD na SAMUEL LUCAS, Picha na Standard Radio FM
No comments:
Post a Comment