Wakazi waishio jirani na mlima Kilimanjaro watanufaika na utalii wa
kuruka milima kwa maparachuti utakaofanyika kwa mara ya kwanza nchini, mwezi
februari mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari, afisa habari wa mamlaka ya Hifadhi
za Taifa Tanapa Bw. Pascal Shelitete amesema fedha zitakazopatikana kupitia
utalii huo zitabaki nchini na wananchi waishio jirani na mlima Kilimanjaro
watanufaika kupitia mradi wa utunzaji mazingira.
Mradi huo ni pamoja na shughuli zinazohusu masuala ya virusi vya
ukimwi, mradi wa maji safi na salama chini ya asasi za one foundation, water
International, na plant purpose.
Tukio hilo linatarajiwa kukusanya zaidi ya watalii mia moja kutoka
nchi ishirini na tano duniani, na imelenga kukusanya takribani shilingi bilioni
mbili za Kitanzania.
No comments:
Post a Comment