On my behalf, Management and staff of STANDARD VOICE LTD
& STANDARD RADIO FM 90.1 Singida, I hereby wish all listeners, Singida
community and all Tanzanians a HAPPY & PROSPEROUS NEW YEAR 2013.
MPENDWA MSIKILIZAJI WA STANDARD RADIO FM
MIMI JAMES JAPHET DAUD, MKURUGENZI MTENDAJI WA MAKAMPUNI YA
BUHANZO INTERPRISES LTD NA STANDARD VOICE LTD AMBAYE NI MMILIKI WA STANDARD
RADIO FM SINGIDA
NINAPENDA KUCHUKUA FURSA HII KUKUPONGEZA SANA KWA KUUFIKIA
MWAKA MPYA WA 2013, NINAWAOMBEA MWAKA HUU UWE WA AMANI, FURAHA, UPENDO NA
UCHAPA KAZI UTAKAOLETA TIJA KWA MAENDELEOO YA MTU MMOJA MMOJA, KAYA, MKOA NA
TAIFA KWA UJUMLA
MIMI PAMOJA NA WAFANYAKAZI WOTE WA MAKAMPUNI YA BUHANZO NA
STANDARD, TUNAPENDA KWA NAMNA YA PEKEE KABISA KUTOA SHUKURANI ZA DHATI KWAKO
WEWE MSIKILIZAJI WA STANDARD RADIO, WAKAZI WOTE WA MKOA WA SINGIDA, UONGOZI WA
SERIKALI, MASHIRIKA YA UMMA NA TAASISI ZA KIJAMII PAMOJA NA VYAMA VYOTE VYA
SIASA, KWA NAMNA MNAVYOIPOKEA NA KUISIKILIZA RADIO YETU.
NDUGU ZANGU UKARIMU WENU KWA STANDARD RADIO NI WA KIPEKEE
KABISA, NINAPENDA KUKIRI KUWA UAMUZI WETU WA KUILETA RADIO HII MKOANI SINGIDA
UMEENZIWA NA WANA SINGIDA VILIVYO, TUMEKUWA TUKIPOKEA MAONI MENGI AMBAYO YOTE
YANADHIHIRISHA MAPENZI MEMA KWA RADIO HII
STANDARD RADIO NI RADIO YA JAMII, YENYE MALENGO YA KUCHOCHEA
MAENDELEO YA JAMII KWA NJIA YA KUHABARISHA, KUELIMISHA NA KUBURUDISHA, MALENGO
YETU NI KUISAIDIA JAMII KUIBUA NA KUTEKELEZA SHUGHULI ZA MAENELEO HUSUSANI
KILIMO, BIASHARA, UJASIRIAMALI PAMOJA NA KUHIMIZA MASUALA YA ULINZI NA USALAMA
KUPITIA KAULI MBIU YA ULINZI SHIRIKISHI NA UTII WA SHERIA BILA SHURUTI
JAMII INAPASWA KUPATA FURSA YA KUTOA YALIYO MOYONI ILI VYMBO
VYA MAAMUZI VIYASIKIE NA KUYAFANYIA KAZI, JAMBO HILI NI GUMU KAMA HAKUNA CHOMBO
MBADALA CHA KUFIKISHA SAUTI YA WANANCHI. HII NDIYO SABABU SISI TUMEKUJA SINGIDA
ILI TUWE SAUTI YA WASIO SIKIKA, KAMA KAULI MBIU YETU INAVYO SEMA (THE VOICE
OF VOICELESS)
STANDARD RADIO BADO IKO KATIKA MCHAKATO WA MWISHO
KUELEKEA KUANZA MATANGAZO RASMI KWA MUJIBU WA TARATIBU ZA MAMMLAKA YA
MAWASILIANO TANZANIA, KWA HIYO TUNAKUOMBA NDUGU MSIKILIZAJI UENDELEE KUWA NA
SUBIRA KWANI WAKATII WOWOTE MATANGAZO YETU YATAANZA KUSIKIKA KWA NJIA YA
VIPINDI MBALIMBALI.
SUBIRA YAVUTA KHERI, TUMEVUMILIA TANGU ENZI ZA UKOLONI NA
BAADA YA UHURU MIAKA HAMSINI ILIYOPITA SINGIDA IKIWA HAINA RADIO, SASA TUSISHINDWE
KUVUMILIA KIPINDI HIKI KIFUPI KIJACHO AMBACHO STANDARD RADIO INAJIWEKA SAWA ILI KUKULETEA
MATANGAZO KAMILI
NARUDIA TENA KUKUSHUKURU NA KUKUTAKIA MWAKA MPYA MWEMA
MUNGU AWABARIKI
No comments:
Post a Comment