Na Edilitruda Chami
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewataka wananchi wa mkoa wa Singida
kushiriki kikamilifu katika shughuli za kilimo, ili kuondokana na umaskini.
Wito huo ameutoa jana katika ibada ya kumuweka wakfu askofu
wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania KKKT mkoani singida, Dr.Alex Nkumbo
iliyofanyika katika kanisa la msalaba mrefu {EMMANUELI} manispaa ya singida
Ameongeza kuwa kwa kufanya hivyo umaskini utatoweka na kwamba ni vyema wakatambua kuwa kilimo
hakichagui mtu, kabila wala dini ila ni juhudi za mtu binafsi hivyo washikamane
ili kuleta maendeleo kupitia kilimo
Ametaja mazao ambayo hustawi
vizuri mkoani Singida kuwa ni alizeti, vitunguu, na pamba ambapo wengi wamekuwa
hawajishughulishi na kilimo hicho.
Wakati huo huo, askofu mpya wa
KKKT usharika wa Emanuel dayosisi ya Kati Singida, Dr.Alex Nkumbo amekiri kufuata
sheria za kanisa hilo mbele ya waumini na viongozi
wa kanisa hilo nchini.
Amesema kuwa atakuwa mvumilivu, jasiri, na mwenye moyo wa
kujitolea kwa mujibu na taratibu za nchi
pamoja na kanisa hilo atatekeleza majukumu yote yaliyo ndani ya uwezo wake
ikiwemo kuhimiza waumini kaushiriki katika shughuli za kilimo ipasavyo ili
kunyanyua uchumi nchini Tanzania
Aidha maaskofu pamoja na
wachungaji wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania wamempokea kwa furaha na amani na kumhakikishia
kuwa watampa ushirikiano kiongozi huyo katika
njanja mbalimbali za kimaendeleo mkoani singida na kuwa atakayekiuka na kuwa
tofauti na dini yao atakuwa kinyume na matakwa yao kwani moja ya lengo la
kanisa lao ni kuhimiza kilimo na kuhakikisha kila muumini anajishughulisha na
kilimo
Waumini waliohudhuria katika
ibada hiyo wamewashukuru viongozi wa serikali waliohudhuria katika ibada hiyo, bila
kujali dini zao kama vile mkuu wa mkoa wa singida Dr Paseko Kone, Mh. Mohamed Dewji
ambaye ni mbunge wa Singida,. wakuu wa wilaya, wabunge na watumishi wa serikali
mkoani humo.
No comments:
Post a Comment