Watu 12 wanaotuhumiwa kuwa wahamiaji haramu kutoka
nchi za Ethiopia na Somalia wamekamatwa na idara ya uhamiaji mkoani Singida
wakiwa njiani kuelekea Afrika ya kusini
Kaimu Mkuu wa idara ya uhamiaji mkoani Singida bw.
Joseph Mshana amesema wahamiaji hao wamekamatwa jana katika eneo la
Kititimo manispaa ya Singida kwa msaada
wa raia wema wakiwa wamejificha vichakani
Kamanda Mshana amesema kuwa wahamiaji watatu
wanatoka Somalia na wengine tisa wanatoka Ethiopia na kwamba walikuwa wakisafiri
kwa kutumia basi la kampuni ya Mtei express.
Mmoja wa wahamiaji hao kutoka Somalia Bw. Ahmedi
Mohamedi amesema, walikuwa wakitoka
katika nchi zao kuelekea Afrika ya kusini wakipelekwa na watu wasiowafahamu
kutafuta kazi kutokana na hali ngumu ya
maisha iliyo katika nchi zao
Idara ya Uhamiaji kwa kushirikianan na jeshi la
polisi wamewafikisha wahamiaji hao mahakamani ya ambapo watasomewa mashtaka
yanayowakabiri ya kuingia nchini kinyume cha sheria za uhamiaji
No comments:
Post a Comment