Na Nathaniel Limu
JUMLA ya raia 12 raia wa nchini Ethiopia,wamehukumiwa na mahakama ya wilaya
ya Singida,kulipa faini ya shilingi laki moja (100,000) kila mmoja baada ya kukiri
makosa mawili ya kuingia na kuishi ndani ya ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania bila kibali halali.
Pia mahakama hiyo,imeamuru basi la kampuni ya Mtei ya mjini Arusha T.797
CDZ lililokuwa limebeba Waethiopia hayo,likamatwe na kutaifishwa kuwa mali ya
serikali.
Raia hao wa Ethiopia ambao ni bado vijana wadogo na wengine ni wanafunzi wa
shule na vyuo, ni pamoja na Ahmed Mohammed Mahamud,Tazana Dijamo Walao, Mohammed
Abdi Osman, Abraham Nirato Shango, Adinan Abrahim Abdalah na Alamu Ayele Gabresekesie.
Weingine ni Muhidini Sufiani Ahmed, Tasfai Sutatu Kidisu, Yassin Mohammed Hassan,
Afandi Aden Suleiman, Ayele Liranso Gafuche na Pakala Agore Mancha.
Baada ya nwendesha mashitaka mwanasheria wa serikali Ahmed Seif kuwasomea
makosa hayo mawili ya kuingia na kuishini nchini bila ya kuwa na
kibali,washitakiwa wote kila mmoja kwa nafasi yake, walikiri kutenda makosa
hayo.
Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo,mwanasheria wa serikali,Seif,aliiomba
mahakama hiyo kuwa iwape adhabu kali washitakiwa ikiwa ni njia moja wapo ya
kukomesha vitendo vya wahamiaji haramu kuingia na kuishi nchini bila ya kuwa na
kibali cho chote halali.
"Mheshimiwa hakimu vile vile naiomba mahakama yako itaifishe basi la
Mtei lililotumika kuwasafirisha wahamiaji hawa haramu ili kuwaogofya wenye
magari kuacha kusafirisha raia wa kigeni wasiokuwa na kibali halali cha kuingia
na kuishi nchini"alisema Seif.
Akitoa hukumu hiyo, hakimu mfawidhi kiongozi wa mahakama ya wilaya ya
Singida, Flora Ndale,alisema mahakama yake imezingatia yale yote yaliyoombwa na
upande wa mashitaka na utetesi na kufikia uamuzi wa kutoa adhabu ya kulipa
faini ya shilingi laki moja kwa kila mshitakiwa.
"Mahakama hii inawatia hatiani na kuwapa adhabu ya kulipa faini hiyo
ya shilingi laki moja kila moja na atakayeshindwa kulipa faini,atakwenda
kutumikia jela kwa kipindi cha miezi mitatu"alisema hakimu Ndale.
Hata hivyo,washitakiwa wote 12,kila mmoja wao alilipa faini hiyo ya
shilingi laki moja na hivyo kuachiwa huru.
Kwa mujibu wa mwanasheria wa serikali Seif, washitakiwa hao wamekamatwa January
17 mwaka huu alasiri katika eneo la kijiji cha Kititimo nje kidogo ya mji wa
Singida wakiwa wametokea mkoani Arusha wakielekea nchini Afrika kusini.
No comments:
Post a Comment