Na Edilitruda Chami & Abdul Bandola.
Zaidi ya watu laki moja na ishirini na tisa elfu mkoani Singida wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa chakula.
Hayo yamebainishwa na kaimu mshauri wa idara ya kilimo mkoani Singida Bw. Lucas Nkuki wakati wa kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika jana katika ukumbi wa manispaa ya Singida.
Bw. Nkuki Amesema kuwa, tathimini iliyofanywa imebaini kuwa zinahitajika tani 1,292 za chakula
mchanganyiko kwa halmashauri ya wilaya ya Ikungi, tani 1,184 kwa halmashauri ya wilaya ya Manyoni, huku tani 711 zikihitajika katika Manispaa ya
Singida na tani 1296.2 katika halmashauri ya wilaya ya Singida.
Kutokana na hali hiyo Baraza la Madiwani la halmashauri ya
wilaya ya Singida wametoa muda wa siku tano kwa Mkurugenzi
wa halmashauri iyo kuhakikisha analitafutia ufumbuzi tatizo la upatikanaji
wa chakula, la sivyo wataunda tume
kwenda kwa Waziri Mkuu.
Zaidi ya kaya thelathini elfu zinahitaji chakula cha msaada
mkoani humo, na hadi sasa wilaya za Iramba na Manyoni zimepata chakula hicho,
ingawa hakikutosheleza mahitaji.
Mkoa wa Singida una wilaya sita ambazo ni Singida mjini,
Singida vijijini, Mkalama, Iramba, Manyoni
na Ikungi.
No comments:
Post a Comment