Na. Halma Jamali
Singida
Mtu mmoja mkazi wa Kiomboi mkoani Singida Mkapa Jumanne 18,amefariki dunia papo
hapo baada ya kurukia gari lililokuwa kwenye mwendo kasi.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa Linus Sinzumwa amelitaja
gari hilo kuwa ni Mini Bus Fuso lenye namba za usajili T.590 ABA lililokuwa
linatoka maeneo ya Kinampanda madukani kuelekea Haydom katika wilaya mpya ya
mkalama.
Alisema kuwa marehemu huyo ambaye ni konda wa gari hilo juzi
tar 14,majira ya saa 9 alasiri alikuwa katika harakati za kupanda gari hilo
wakati lipo kwenye mwendo na bahati mbaya alitereza na kuangukia katika tairi la
nyuma la gari hilo na kupitiwa na kufariki papo hapo.
Aidha Sinzumwa
alisema kuwa dereva wa gari hilo aliyejulikana kwa jina la Hereio Neema
42,anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi.
Kamanda huyo
ametoa wito kwa madereva wanaoendesha vyombo vya moto kuwa makini ili kuepusha
vifo vya watu wasio na hatia.
No comments:
Post a Comment