NA HALIMA JAMAL
Rais kwa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk Jakaya mrisho kikwete
amewataka viongozi wa dini kuhubiri amani ya nchi kwenye kila ibada ili kuokoa
amani ya nchi inayoyumba kwa sasa.
Kikwete ametoa wito huo jana wakati wa sherehe ya kusimikwa wakfu kwa
askofu wa jimbo ya kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania mkoani Singida
askofu Dk Alex Seif Mkumbo.
Alisema kuwa miaka ya hivi karibini kumekuwepo na uvunjifu wa amani na
vurugu zisizokuwa na maana kutokana na kutofautiana kwa dini na baadhi ya watu
kuona dini waliyokuwa nayo wao ni zaidi ya wenzao na kuwa dini ni imani ya
mtu.
Aidha Kikwete alisema kuwa viongozi wa dini zote wanawajibu mkubwa kwa
kipindi hichi kuokoa taifa kwa kutoa tofauti kati ya dini na dini ila bila
kutekeleza wajibu huo tofauti hizo hazitakwisha.
Dk Kikwete alisema kuwa anapata hofu kubwa kwa watu ambao hawana heshima ya
kuwasikiliza viongozi wao wa dini na kufuata mambo ya dunia na kuchochea vurugu
katika nchi yao wenyewe.
''nawaomba nyie viongozi wa dini mtumie karama mliyopewa na mwenyezi mungu
kulinusuru taifa letu lisiangamie kutokana na watu wachache,kwani watu hawa
tunaowaongoza ni wetu sote kwa upande wa kiroho ni ninyi viongozi wa dini,na
sisi serikali tunaongoza kwa maendeleo ya taifa'',alisema Dk Kikwete.
Kikwete aliwataka viongozi hao kutokata tamaa kuhubiri amani ya nchi kwani
binadamu wanaowahubiria wako tofauti.
Sanjari na hilo dk Kikwete amempongeza askofu aliyepewa wakfu huo na kumpa
moyo wa kufanya kazi yake aliyopewa na mungu kwa umakini na upendo.
''nakupongeza sana kwa kupewa cheo hicho kwani waliokuchagua wanajua kuwa
utawaongoza kwa kufuata miongozo ya mungu na kutangaza dini yako wa watu wote na
na kuahidi kushirikiana na mataifa makubwa ya dini ili kuweza kujenga amani ya
nchi yetu kwa pamoja tunaweza'',alisema Kikwete.
Kwa upande wake askofu Mkumbo alisema kuwa anamshukuru mungu kwa kumpa
wakfu wa kuwatumikia wakristo wa kanisa lake lililoanzishwa mnamo mwaka
1911.
Alisema kuwa amedhamiria kupambana na changamoto zote zinazoikabili amani
ya taifa lake na kuhakikisha zinapungua na kumalizika kabisa.
Aidha askofu Mkumbo ameomba ushirikiano kwa watu wote ili wale wote
waliokuwa na mpango wa kuvunja amani ya nchi washindwe.
Sherehe hizo zimefanika katika viwanja vya kanisa la KKKT katika manispaa
ya Singida na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kidini na serikali.
No comments:
Post a Comment