Friday, January 18, 2013

WAHAMIAJI KUTOKA SOMALIA NA ETHIOPIA WAKAMATWA


Watu 12 wanaotuhumiwa kuwa wahamiaji haramu kutoka nchi za Ethiopia na Somalia wamekamatwa na idara ya uhamiaji mkoani Singida wakiwa njiani kuelekea Afrika ya kusini

Kaimu Mkuu wa idara ya uhamiaji mkoani Singida bw. Joseph Mshana amesema wahamiaji hao wamekamatwa jana katika eneo la Kititimo  manispaa ya Singida kwa msaada wa raia wema wakiwa wamejificha vichakani

Kamanda Mshana amesema kuwa wahamiaji watatu wanatoka Somalia na wengine tisa wanatoka Ethiopia na kwamba walikuwa wakisafiri kwa kutumia basi la kampuni ya Mtei express.

Mmoja wa wahamiaji hao kutoka Somalia Bw. Ahmedi Mohamedi amesema,  walikuwa wakitoka katika nchi zao kuelekea Afrika ya kusini wakipelekwa na watu wasiowafahamu kutafuta kazi kutokana na hali ngumu  ya maisha iliyo katika nchi zao

Idara ya Uhamiaji kwa kushirikianan na jeshi la polisi wamewafikisha wahamiaji hao mahakamani ya ambapo watasomewa mashtaka yanayowakabiri ya kuingia nchini kinyume cha sheria za uhamiaji

No comments: