Na Beatrice Mosses.
Mkurungenzi wa manispaa ya Singida Bw. Mathias Mwangu
ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wafanya biashara hao, kuwa eneo hilo limekuwa dogo na
bidhaa ni nyingi.
Baadhi ya wafanya biashara wa zao hilo wameiomba Manispaa iwajengee vibanda
hata viwili vitakavyotumika kulipia ushuru.
Hata hivyo miundombinu katika soko la Misuna kama vyoo na vibanda bado havijakamilika, Bw. Mwangu
amesema Manispaa itakamilisha miundombinu hiyo haraka ili soko la Misuna lianze
kutumika.
Soko la Ukombozi litaendelea kuwepo kwa ajili ya kuuzia kuku
na bidhaa nyingine ndogondogo.
No comments:
Post a Comment