ACP Linus Sinzumwa Kamanda wa polisi mkoa wa Singida
Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema ametoa
jumla ya piki piki 22 kwa jeshi la polisi mkoani Singida, kama sehemu ya
utekelezaji wa mkakati wa kuimarisha ulinzi nchini na kusogeza huduma za
usalama jirani na wananchi
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkuu wa jeshi
la polisi mkoa wa Singida ACP Linus Sinzumwa amebainisha kuwa pikipiki hizo
zitasambazwa katika tarafa za mkoa huo
Kamanda Sinzumwa amebainisha kuwa piki piki hizo
zitakabidhiwa kwa askari wateule ambao watazitumia kwa ajili ya kufanya doria
na kuzuia uharifu katika tarafa ambazo watapangiwa pamoja na kuimarisha
ushirikiano baina ya raia na jeshi hilo
Mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone,
anatarajiwa kukabidhi vyombo hivyo vya usafiri kwa jeshi hilo mapema wiki ijayo
No comments:
Post a Comment