KAMANDA
wa Polisi mkoani Tabora ACP Anthony Rutta amesema kuwa atayafungia kufanyakazi
makampuni yote ya ulinzi mkoani humo ambayo yanashindwa kutekeleza masharti
yaliyopewa na jeshi hilo.
Mkuu
huyo wa Polisi mkoa wa Tabora amesema kwamba jeshi la Polisi lilitoa masharti
kwa wamiliki wa makampuni yaho kuwa hayaruhusiwi kuajiri walinzi wasio
waadilifu ambao wamekuwa wakila njama za kufanya uharifu wa wizi kwenye taasisi
mbalimbali ambayo wameingia nazo mkataba wa ulinzi.
Akizungumza
na mwandishi wa habari ofisini kamanda Ruta alikiri kuwepo kwa baadhi ya
makampuni ya ulinzi ambayo hayafuati taratibu za ajira za walinzi huku akiapa
kuyashughulikia ipasavyo kwakuwa baadhi ya makampuni hayo yamekuwa yakiajiri
walinzi wasio na sifa na kukosa uaminifu.
Kuhusu
matukio ya hivi karibuni ya wizi uliofanyika katika Shirika lisilo la
kiserikali la Total Land care ambalo lilipata hasara ya zaidi ya shilingi
mil.kumi na tatu baada ya walinzi wa kampuni ya ulinzi ya Alliance Day &
Night la hapa mjini Tabora ambao wanadaiwa kula njama na kufanya wizi wa
kuvunja ofisi za Shirika hilo.
Kamanda
Rutta amesema bado Polisi wanaendelea na uchunguzi lakini mlinzi mmoja wa
kampuni hiyo anayefahamika kwa jina la Said Kayungilo alitoweka kabla ya kukamatwa.
No comments:
Post a Comment