Mkuu wa mkoa wa Singida Dr, Parseko Kone ameonya tabia ya
baadhi ya maafisa wa serikali na vyombo vya habari kutoa taarifa zisizo sahihi
kwa wananchi
Dr. Kone amesema hayo jana katika hafla fupi ya kuuaga mwaka
2012 na kuukaribisha mwaka 2013, iliyofanyika katika chuo cha utumishi wa Umma
mjini Singida
Dr. Kone amesema hayo kufuatia vyombo vya habari kuripoti
habari ya uhaba wa chakula mkoani Singida, na kutaja kuwa takwimu zilizotolewa
katika habari iliyochapishwa na moja ya magazeti ya kil asiku si sahihi
Mwishoni mwa wiki, baraza la madiwani wilaya ya Singida
lilikiri kuwepo kwa uhaba mkubwa wa chakula na kuagiza uongozi wa halmashauri
hiyo kulitafutaia ufumbuzi mara moja
1 comment:
Mheshimiwa, sasa huyo mkuu wa mkoa mbona haeleweki?Baraza la madiwani limesema kuna njaa,yeye anakanusha tushike lipi?
Post a Comment