Tuesday, January 29, 2013

MABINTI WASHAURIWA KUSUSIA NDOA DHIDI YA VIJANA WASIO NA NYUMBA BORA

Mkuu wa wilaya ya Mkalama Bw. Edward Ole Lenga (kulia) akisisitiza jambo kuhusu ujenzi wa nyumba wilayni humo na kuwataka wavulana wasikimbilie kuoa wakati wakiishi ndani ya Tembe, Tembe ni aina ya mjengo wa asili kwa wakazi wa mikoa ya kati, hususani Singida, Dodoma na sehemu ya miko aya Tabora na Shinyanga.

Serikali wilayani Mkalama mkoani Singida imewataka wasichana kukataa kuolewa na wanaume ambao hawajajenga nyumba za kisasa kama sehemu ya kuhimiza ujenzi wa nyumba bora

Ushauri huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Mkalama Edward ole Lenga wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kwa kipindi cha mwaka 2005 hadi 2012

Bw. Lenga amesema bado wakazi wa wilaya hiyo mpya hawajawa na mwamko wa kujenga nyumba bora na badala yake wanaendelea kuishi katika nyumba za asili maarufu kama tembe

Amesema nyumba hizo za asili si imara na zimekuwa zikihatarisha maisha ya wananchi hasa nyakati za masika
Mkuu huyo wa wilaya amebainisha kuwa serikali licha ya kuhimiza wananchi kujenga nyumba bora bado mwitikio ni mdogo na hivyo kuwaelimisha wasichana na akina mama juu ya umuhimu huo, ndiyo njia pekee ya kuleta mabadililo   

2 comments:

Anonymous said...

Mkuu wa wilaya mhe. Lt edward ole Lenga alimaanisha kuwashauri vijana kuachana na Nyumba za tembe

Anonymous said...

Mkuu wa wilaya ya mkalama alimaanisha kuwashauri vijana kuwa msichana asikubali kuolewa na mvulana ambaye hana mkakati wowote juu ya kujenga nyumba bora,kampeni hii itasaidia kuondokana na nyumba za tembe