Friday, August 31, 2012

SINGIDA PRESS CLUB YAPEWA SOMO


Na Evarista Lucas

Singida

 

 

Mkuu  wa wilaya ya Iramba  Bwana Yahya   Nawanda; amewaasa viongozi na wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari Singida(SINGPRESS  kuyafuata yale waliyoafikiana katika mkutano na kuhakikisha kuwa hawaendi kinyume na mabadiliko hayo.

Akihutubia wanachama hao katika mkutano wao wa marekebisho ya katiba ya SINGPRESS uliofanika katika kijiji cha Kiomboi wilaya ya Iramba mkoani Singida; Nawanda aliwawataka wanachama hao kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa kufuata maadili ya kazi yao.

“Siku hizi tasnia ya uandishi wa habari imekuwa inaingiliwa sana na watu na watu wasiokuwa na maadili  ambao ndio wanaofanya kazi hii na heshima mbele ya jamii, kwani uandishi ni maadili.” Alisisitiza Nawanda.

 

Kwa upande mwingine Nawanda aliwataka wanachama hao kuepukana na ushabiki wa kisiasa ili waweze kufanya kazi yao kwa ufanisi zaidi na kwa kuzingatia maadili ya kazi yao.  “Baadhi yenu mmekuwa wanasiasa tena wa wazi wazi. Mnafanya kazi ya  viongozi wa siasa. Mimi nawaasa mfuate maadili ya uandishi wa habari na kuachana na siasa.” Nawanda.

           

Licha  ya hayo  Nawanda aliwaomba wanachama hao kuandika pia mambo mazuri ambayo yamefanyika hapa mkoani ikiwemo ujenzi wa hospitali ya kisasa ya rufaa, barabara za lami na makazi bora.

 

“Tutawapa ushirikiano mkubwa waandishi wa habari kwani nyie ni watu muhimu kuhabarisha Watanzania kile tunachokifanya katika maendeleo ya mkoa wetu. Wasaidieni kuandika makundi maalumu kama   vile walemavu, changamoto zao na ustawi wao kwa ujumla na sio kujikita kwenye siasa tu. Sasa Tanzania tunajua mwandishi bora ni yule anayejikita kwenye siasa tu.”  Nawanda

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa SINGPRESS Bwana Seif Takaza alimshukuru mkuu huyo wa wilaya  kwa kuitikia wito wa kuwa mgeni wa heshima katika mkutano wao na pia kwa kuwapatia ukumbi uliowawezesha kuikamilisha kazi hiyo muhimu kwa maendeleo ya Klabu.

 

 “Hii ni awamu ya pili kwa waandishi wa habari kufika katika wilaya ya Iramba  awmu ya kwanza ilikuwa ni Mei 3 mwaka huu siku ya uhuru wa vyuombo vya habari ambapo tulikwenda kwa Wahadzabe na kutoa msaada wa chakula na vifaa vya shule. Leo tena awamu ya pili tunafanya mkutano huu hapa.

 

 Katika mkutano huo uliojumuisha wanachama kumi na saba (17) wa SINGPRESS wanachama walipata fursa ya kuipitia kwa umakini katiba hiyo na baadhi ya vipengele vilivyoongezeka katika katiba hiyo.”

No comments: