Monday, August 20, 2012

BROTHERS OF CHARITY NA MAGONJWA YA AKILI



Br. Welhard Mukesha ambaye ni mkuu wa kituo cha afya ya akili kinachomilikiwa na shirika la Brothers of Charity Marumba mkoani Kigoma akiwa katika moja ya majukumu yake ya kutoa huduma za afya ya akili kwa wagonjwa


Na. Prosper Kwigize

Magonjwa ya akili ni moja ya changamoto zinazolikabilii bara letu la afrika na hivyo kuchangia kuzorota kwa maendeleo ya jamii na hasa kaya zenye wagonjwa wa akili

Kwa mujibu wa Takwimu za Kanisa Katoliki nchini Tanzania zaidi ya wagonjwa 68,000 wamepatiwa huduma za afya ya akili katika kituo cha shiopokelewa rika la kitume la Brothers of Charity kilichoko Marumba mkoani Kigoma ambapo 25,000 kati yao ni wagonjwa waliolazwa na kisha kuruhusiwa baada ya akili zao kupata nafuu

Aidha jumla ya wagonjwa wa akili 43000 wamepata huduma kwa nyakati tofauti wakitokea nyumbani ambapo ama wanakuja na kupewa dawa na maelekezo ya matumizi wakiwa majumbani mwao

Hata hivyo Br. Welhard Mukesha ambaye ni mkuu wa kitengo cha tiba ya afya ya akili Marumba anafafanua kuwa, kutokana na changamoto mbalimbali jumla ya wagonjwa wa akili 24 wanalazimika kuishi maisha yao yote katika kituo cha Marumba

Br. Mukesha anabainisha kuwa wagonjwa hao wataishi kituoni hapo kutokana na ama kutengwa na jamii, kutokuwa na ndugu wa kuwalinda na kuwapa huduma za kijamii pamoja na wengine kuwa na ugonjwa sugu wa akilii ambao ulitokana na kucheleweshwa kupata huduma ya matibabu.

Jamii imekuwa na mitazamo tofauti kuhusu magonjwa ya akili hali inayosababisha mikakati ya kupambana na magonjwa hayo ikiwa ni pamoja na vyanzo vyake kushindikana kuzuiliwa kikamilifu na hivyo jamii kuendelea kuathirika.

Moja ya sabau zinazotajwa kuchangia kuwepo kwa magonjwa na wagonjwa wa akili ni matumizi ya madawa ya kulevya na ulevi wa pombe za kupindukia hususani pombe za kienyeji na zile za viwandani maarufu kama Viloba n.k

Ipo hoja pia kuwa magonjwa ya akili chanzo chake ni Kurogwa au kurithi kutoka kwa wazazi au ndugu yeyote katika ukoo

Ssehemu kubwa ya jamii imekuwa ikikimbilia kwa waganga wa jadi kwa ajili ya kutafuta tiba ya magonjwa ya akili lakini kwa bahati mbaya ni wachache wanaopona hususani wale wanaopata ugonjwa huo kutokana na matatizo ya kisaikolojia na matumiziz ya madwaya ya kulevya au ulevi wa pombe kupindukia

Ukosekanaji wa vituo vingi vya tiba ya akili yaweza kuwa chanzo cha kudumu na kuendelea kuwepo kwa dhana potofu ya waganga wa jadi na kuendelea kuzagaa kwa vijana wengi wa kike na wakiume katika mitaa wakiwa wagonjwa na wahanga wa matatizo ya afya ya akili barani afrika

Shirika la Kidini la Brothers Of Charity la Kanisa katoliki limeanzisha kituo cha afya ya akili mkoani Kigoma na tayari wagonjwa wengi wamepata tiba na wengine wanaendelea kupata huduma hiyo na kupona. Inaelezwa kuwa wakati mwingine si wote wanaohitaji kupatiwa madawa bali ushauri nasaha, kupumzishwa kwa muda na kuwapa shughuli ndogondogo kunawawezesha akili yaoo kuwa vizuri na hatimae kurejea katika afya yao ya kawaida

Pichani ni Bw. Mathias Richard mwenye umri wa miaka 32 ni mmoja wa wagonjwa wa akili wanaopatiwa matibabu katika kituo cha Brothers of Charity Marumba mkoani Kigoma- yeye anakili kuwa kama asingeletwa katika kituo hicho angekuwa barabarani akifanya matendo ya wehu na wendawazimu

Picha ya pilii ni Bw. Salila Josephat Msigwa, mwenye umri wa miaka 36, yeye anamuuguza ndugu yake ambaye baada ya kutangatanga kwa waganga wa jadi aliamua kumpeleka katika kituo cha afya ya akil Marumba; sasa anakili kuwa ni vijana wengi wenye matatizo ya akili lakini hawajafikishwa kwenye vituo vya tiba. Msigwa anadai pia kuwa wengi wa wenye matatizo ya afya ya akili chanzo kikibwa ni matumizi ya madawa ya kulevya, bangi na pombe kali, ingawa anakubali pia kuwepo kwa magonjwa ya kurithi pamoja na kurogwa.

PICHA 3. Bw. Nicolaus Edward muugizi wa kituo cha afya ya akili Mrumba mkoani Kigoma, yeye anakil kuwa wengi wa wagonjwa wanaopokelewa katika kituo chao ni vijana wanaotumia madawa ya kulevya hususani Bangi pamoja VILOBA, aidha hisia ya kurogwa ipo na kwamba haina ukweli kwa kiasi kikubwa, anakili pia kuwa yapo matatizo ya akili yanayotokana na urithi na kwamba tatizo kubwa lililopo ni jamii kutowapeleka katika vituo vya afya kupata tiba ba badala yake kuwaacha wakizagaa mitaani.

No comments: