Wednesday, August 15, 2012

UDINI NA SENSA MKOANI SINGIDA


Na, Doris Meghji
Singida

Wasimamizi na makarani wote wa sensa ya watu na makazi wilayani Manyoni wametakiwa kuzingatia maadili ya kazi,ushrikiano wa karibu kati ya wasimamizi, makarani na viongozi wa ngazi zote ikiwa ni pamoja na kujiepusha na masuala ya ushabiki wa kisiasa na kidini kwani takwimu zitakazokusanywa zitatumika kwa ajili ya maendeleo na sio vinginevyo

 Akifungua mafunzo ya wasimamizi na makarani wa sensa wilayani Manyoni jana Mkuu wa wilaya wa Manyoni Bi Fatuma Toufiq amewataka wasimamizi na makarani wa Sensa ya watu na Makazi wilayani humo kuzingatia mambo muhimu ya msingi ili kufanikisha zoezi hilo  wilaya humo.

 Aidha amewataka kuzingatia maadili ya kazi kwa muda wote wa zoezi hilo la sensa ikiwemo kuvaa mavazi ya heshima na yanayokubalika ili wasiwakwaze wananchi wakati wa kuhesabiwa

Bi Toufiq “ushirikiano wa karibu (team work) ni muhimu kati ya wasimamizi,makarani na viongozi wa ngazi zote ni muhimu katika kufanikisha zoezi hili” alisisitiza Mkuu wa wilaya huyo.

Hata hata hivyo amewataka kuacha mahusiano yatakayohatarisha utendaji kazi ikiwa ni pamoja na suala la kujihusisha na ushabiki wa kisiasa na kidini kwani takwimu zitakazokusanywa zitatumika kwa ajili ya shughuli za maendeleo na sio vinginevyo


Suala la kuwa namikini na vyombo vya habari halikusahaulika ambapo Bi Fatma Toufiq amewataka wasimamizi na makaraini hao kuwa makini na vyombo hivyo kwani msemaji mkuu wa masuala ya sensa katika wilaya ni mkuu wa wilaya au Mratibu wa Sensa wa wilaya tu.

 Awali akitoa taarifa ya mafuzo kwa mkuu wa wilaya ya Manyoni mratibu wa sensa ya watu na makazi wilayani manyoni Bwana Edga Madeje  amesema jumla washiriki mia nane sabini na tisa (879) wanapatiwa mafunzo ambapo wasimamizi 66, makarani waandamizi 460 na makarani 353.

Hivyo amewataka washiriki wa mafunzo hayo kutumia fursa hiyo ya mafunzo kuzingatia kwa makini mambo yote wanayofundishwa na wakufunzi wakati wote wa kipindi cha mafunzo kwa kuzingatia umuhimu wa kipekee wa sense ya mwaka huu ambapo takwimu zake zitatumika kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa malengo ya millennia ya mwaka 2015 na program mbali mbali za maendeleo nchini

 Aidha takwimu hizo pia zitatoa viashiria vitakavyotumika katika kufuatilia na kutathimini Dira za Taifa za maendeleo 2025 kwa Tanzania bara na mwaka 2020 kwa Tanzania Zanzibar ikiwa ni pamoja na mikakati ya  kukuza uchumi na kupunguza umaskini kwa Tanzania bara na MKUZA kwa Tanzania Zanzibar alieleza Mratibu wa sensa Bwana Madeje.

 Mafunzo hayo ya makarani wa sensa ya watu na makazi yameanza Agosti tisa ambapo mafunzo ya dodoso refu yatakuwa ya muda wa siku 10 na dodoso fupi yakuwa ya muda wa siku 7

Mwisho

No comments: